DARASA/CHUMBA CHA MAFUNDISHO: ''Mkalimani Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY. (Darasa linaendelea lilipoishia...) "Hebu angalia midomo yako imesema nini na nini? Umekiri nini na hujatimiza, umedanganya mbele ya MUNGU aliye HAI. Ni vizuri angalia hicho kinywa hakijaropoka chochote. Biblia inasema, “Mpende jirani yako kama nafsi yako”, hivyo kabla hujampenda mtu anza kujipenda mwenyewe. Kama wewe unateseka ni ngumu kumsaidia mwingine. Kama unahubiri Baraka, lazima tuzione hizo Baraka kwanza kwako ndipo tupokee na sisi. Ukidhamiria ndani ya moyo wako na kuyatendea kazi haya uyasomayo, YEYE ni wa KWELI na ATAKUWEZESHA kuijua KWELI na Ukishajua KWELI utakuwa HURU KWELI KWELI."" (Darasa linaendelea...)

Comments