"Kubali kumtumikia MUNGU; Muabudu MUNGU hapigwi na adui, Muabudu MUNGU hasumbuliwi na adui, Muabudu MUNGU hakosi chakula. Mfanya Ibada analindwa, Mfanya Ibada anazungukwa. Akaniambia, ‘’Nimekupa Huduma ndani yako ya kuhamishia’’. Pia, wakati huo huo, alinifanyia vitu kadhaa. Aliyashika macho yangu, akatoa vigamba vigamba na kusema, ‘’Kuanzia sasa, utaona mambo ya Ki-Ungu. Mambo yaliyo katika ulimwengu wa roho’’. Akanishika mikono na kuambatanisha na mikono yake. Alipotoa mikono yake, nikaingalia mikono yangu nikaona damu. Akasema, ‘’Nimeitakasa mikono yako, ili kila utakalolifanya likafanikiwe, na kila utakayemwekea mikono, akafunguliwe’’. Kiisha kwenye macho akaweka Malaika, mmoja asimame upande huu na mwingine upande huu – walinde macho yangu usiku na mchana, ili kuweza kuona njia ya kwenda na kitu cha kufanya kwa ajili ya BWANA, na kwa ajili watu wake wanaokuja kwa ajili ya kumjua BWANA. Kisha akayagusa masikio yangu na kusema, ‘’Kuanzia sasa, utaisikia sauti yangu kwa usahihi’’. Kwenye kinywa, akanifanyia kitu cha ajabu sana! Akaweka kidole kinywani mwangu, akanigusa na kusema, ‘’KUanzia sasa, NENO limetakaswa kinywani mwako’’. Halafu akanishika miguu yangu katika sehemu ya magoti na akasema, ‘’Umetiwa nguvu miguuni na hata kwenye kiuno’’. Akaongeza kusema, “Utafanya kazi ambayo wengine hawajawahi kufanya’’. Baadae akasema, ‘’Kuanzia sasa, nimeweka mamlaka juu yako, na nguvu na uwezo’’. Akaniambia maneno mengi ya kunitamkia kwamba amenipa Huduma ya kuhamishia ya ‘Kitume’ na ‘Kinabii’. Akasema, “Katika Utume wako, mwangalie sana Paulo alivyopita kimamlaka, itafanana na hilo. Katika Unabii, angalia Isaya alivyotabiri. Utatabiri mambo yajayo mambo ambayo hayajawahi kuwepo bado, wala hayajawahi kutokea, wala hakuna aliyewahi kuyatamka katika kizazi chako na katika jamii yako, na yote yatatimia’’. Akaniambia , “Utaweza kuwahudumia Mitume, Manabii na wenye huduma zingine". : Apostle & Prophet Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.

Comments