Darasani!
"Watu wengi wameishi kwenye Wokovu kwa miaka mingi lakini maisha yao yamekuwa ni ya dhiki na kushindwa pamoja na kujifariji katika hali hizo. Wengi wamesimamia mafundisho na mapokeo ya aina aina lakini hawajasaidika. Safari ya kwenda mbinguni haiishi katika kuokoka tu bali inataka ifanyike kazi kubwa ili kumwandaa na kumkamilisha mtu hadi afikie cheo cha KRISTO. BWANA MUNGU akasema ni YEYE atufundishaye ili tupate faida. Faida ni pamoja na kufika MWISHO MWEMA wa Safari na sio Kufia njiani.
Uzoefu wangu kwenye Utumishi wa BWANA wetu YESU KRISTO umeonyesha kuwa TABIA tulizo nazo zimechangia kwa kiasi kikubwa katika kutofanikiwa kwa Wana wa MUNGU. TABIA tulizo nazo mbali na mambo mengine zimetunyima:
i) Kufanya IBADA na MUNGU wetu ambalo ndilo KUSUDI KUU la kuwepo kwetu chini ya jua.
ii) Mafanikio na Baraka za Kiroho, Kiafya, Kiuchumi, Kindoa na Kimaisha.
iii) Amani na MUNGU na Wanadamu pia.
i) Kufanya IBADA na MUNGU wetu ambalo ndilo KUSUDI KUU la kuwepo kwetu chini ya jua.
ii) Mafanikio na Baraka za Kiroho, Kiafya, Kiuchumi, Kindoa na Kimaisha.
iii) Amani na MUNGU na Wanadamu pia.
Tusipopona katika kurekebisha tabia zetu ni vigumu sana majina yetu kuandikwa katika kitabu cha MWANA KONDOO.
MUNGU anasema na watu wake kupitia njia mbalimbali ikiwemo Maandiko hasa yaliyoandikwa kwa kufunuliwa. Nitafundisha kwa sehemu tabia za Mwanadamu na jinsi anavyoweza kubadilika. Wale WATAKAOFUNGUA MIOYO yao na KUPOKEA yaliyomo humu na KUYAFANYIA kazi, hakika WATAPONA katika maeneo mengi ya Tabia zao za kale.
Omba MUNGU Akupe KUELEWA mambo ambayo yatakusaidia Wewe mwana wa MUNGU kutoka hatua moja hata nyingine hadi kufikia KIMO CHA KRISTO." : Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.
(Itaendelea kesho mwana wa MUNGU, USIKOSE na USIPITWE hata na siku moja, shetani hasikuzuilie Ubadae wako, Mafanikio yako na UZIMA wako wa Milele, mkatae shetani mpingeni naye atawakimbia.)
Mbarikiwe.
Comments
Post a Comment