MANENO YENYE HEKIMA NA UFAHAMU
MANENO YENYE HEKIMA NA UFAHAMU: (Mkalimani Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira). ''MUNGU Anasema, “Wenye Haki wana mateso mengi”! Watu watasema, mbona huyu ana shida sana, mbona yuko hivi na hivi….waambie ni kweli maana wenye haki wana mateso mengi! Wayahudi ni watoto wake MUNGU, na MUNGU Alimwambia Ibrahim Atambariki na Watoto wake wote lakini wakawa Watumwa katika Nchi ya M isri. Wakamlilia MUNGU katika shida zao, katika maangamizo yao Wakamlilia BWANA kwa miaka 400 na BWANA AKAWAOKOA. “Usione nina mateso mengi, yupo ANAYEKUJA KUNIOKOA”! N.B. Kutoka Kanisa kwenda Kanisa, kwenda mikutano mbalimbali ya maombi HAIWEZI Kukutoa kwenye Matatizo mpaka UTAKAPOAMUA KUTOKA KWENYE TATIZO, Mpaka UTAKAPOAMUA na KUAMINI na KUKUBALI KWAMBA HAKI yako INATOKA kwa MUNGU na UNAIPATA kwa Sababu YESU KRISTO AMEKUFA KWA AJILI YAKO na AMELIPA DENI ZAKO ZOTE (Hapo ndipo UTATOKA KWENYE TATIZO). Lakini bila ya kuelewa hivyo, utazunguka Makanisa mengi na Utaombew...