SHUHUDA SHUHUDA SHUHUDA.


MUNGU Wetu na BABA Yetu ni MZURI MNO, Anatupenda sana Wanawe,... Katika YESU KRISTO Bwana na Mwokozi wetu, MUNGU WETU MKUU wa EFATHA,...

Wana wa MUNGU hawa Jane na Denis Mr & Mrs, waliamua leo kuja mbele za Wana wa MUNGU, mbele ya Hema ya BWANA kuja Kushuhudia Matendo MAKUU ya MUNGU WETU na BABA YETU MKUU Aliyowatendea katika Maisha yao. Walioana miaka 5 iliyopita, Lakini katika miaka yote hiyo Hawakuweza kufanikiwa kupata Mtoto, Hospitalini waliambiwa kuwa HAWAWEZI Kupata MTOTO KAMWE, Kwani Hawana MBEGU ZA KUZALISHA Watoto,... Madaktari waliwapima na kuwapa majibu hayo kila Hospitali mbalimbali walizokwenda kutibiwa.

Lakini Hawakukata tamaa,... Walimwamini MUNGU wetu MKUU, MUNGU wa EFATHA kuwa ATAWAPA Watoto,... Kwenye Kusanyiko la wana wa MUNGU la Mwaka jana 2012 Kibaha Precious Centre, Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira aliita Wale wote ambao Hawajapata watoto ili Awaombee,... Huyu mwana wa MUNGU Jane alitoka mbele na kuombewa,... Haleluya... MUNGU wetu BABA wa Efatha SI MUONGO, HASHINDWI KITU,... YEYE ni MUWEZA Wa YOTE, Kila kitu KINAPATIKANA KWAKE Haleluya,...

Oooh Haleluya, ... Leo Wametoka mbele na Kushuhudia MATENDO MAKUU Ya MUNGU WETU na BABA YETU MKUU Wa Efatha,... Wamepata Mtoto,... Ambao Waliambiwa na Madaktari na Wataalamu katika Mahospitali mbali mbali kuwa KAMWE Hawatapata Watoto, lakini LEO Kupitia MUNGU MKUU, MUNGU MUWEZA Wa EFATHA AMEWAPA Watoto kwa JINA la BWANA na MWOKOZI wetu YESU KRISTO,...

Tunamshukuru MUNGU wetu na BABA YETU kwa BARAKA HII, Haleluya katika YESU KRISTO Bwana Wetu.






Haleluya,... MUNGU Wetu na BABA YETU ni Mzuri sana, Anatupenda sana Wanawe
Kijana huyu mwana wa MUNGU, leo aliamua kuja Kushuhudia mbele za Wana wa MUNGU na Mbele za Madhabahu ya MUNGU wetu MKUU, juu ya Matendo Makuu ambayo MUNGU wetu BABA Amemtendea katika Maisha yake,... Kijana Mwana wa MUNGU (Denis Malesela) anashuhudia kwamba, kabla hajaamua Kumpokea BWANA wetu YESU KRISTO Kuwa BWANA na MWOKOZI wa Maisha yake (Kuokoka) alikuwa ni Mlevi sana, Alianza kunywa pombe toka akiwa darasa la tatu, Bibi yake alikuwa anapika pombe kwa hiyo alikuwa anampatia mjukuu wake asubuhi kabala ya kwenda shule na hata akirudi shule.

Kwa hiyo Denis akajikuta roho ya ulevi imemwingia, na hiyo roho imemtesa sana, kwani alikuwa Anakunywa pombe na kupigana na watu, na hata ilifikia pointi akawa anapelekwa polisi na kuwekwa sello kwa sababu tu ya pombe,... Pombe ilimtesa sana.

Denis akaendelea kushuhudia kuwa, ... baada ya Mjomba wake kumshauri na Kumuhubiria Habari Njema za BWANA Wetu YESU KRISTO, na kumleta EFATHA,... ndipo alipoamua KUOKOKA na ... KWELI YESU WETU HADANGANYI,... Bwana wetu YESU KRISTO Alimbadilisha maisha yake na Kumfanya AWE KIUMBE KIPYA, ... na toka siku hiyo POMBE ALIACHA na HANYWI TENA, na Sasa Amekuwa Kijana Mzuri na Anatenda Vema sasa,... na Yuko na Amani na Furaha katika Maisha yake sasa,... Haleluya.... MUNGU Wetu na BABA YETU Ni MZuri sana, YESU ANATUPENDA, ANATUPENDA Sana, Hakuna Jambo GUMU Kwa Bwana na Mwokozi wetu YESU KRISTO,... Haleluya.

USHINDI ni kwa MWANA KONDOO ALIYE HAI... YESU KRISTO MFALME Mwana wa MUNGU, Mwana wa BABA, MUNGU WETU MKUU Aliye HAI.


Comments