MANENO YENYE HEKIMA NA UFAHAMU: (Mkalimani Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira).

ANENO YENYE HEKIMA NA UFAHAMU: (Mkalimani Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira).

''Biblia inatuambia kuwa, bila kujali uwezo wako wa kusali au mahali unaposali, yako maovu yanayokushuhudia ya kuwa umepungua. Tunasoma, “Ijapokuwa maovu yetu yanatushuhudia, lakini utende wewe kwa ajili ya Jina lako, Ee BWANA! Maana kurudi nyuma kwetu ni kwingi, tumekutenda dhambi.” (Yeremia 14:7) Maovu yetu yanatushuhudia kwa sababu moyo wetu umeiacha sheria ya MUNGU na kushika mapokeo ya wanadamu. Na hicho tulichokipokea ndicho kinachotushuhudia leo.

- Mfano:- Moyo una maandalio, au kitu unachotafuta lakini mara yanapotokea matatizo mtu huyu anaweza kufuta kila kitu chema kutoka kwa MUNGU kutokana na jinsi anavyo kabiliana na changamoto hizo Imeandikwa, “Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu, lakini jibu la ulimi hutoka kwa BWANA” (Mithali 16:1). Biblia inatufundisha kuwa wakati wana wa Israeli walipokuwa wakirudi katika nchi yao ya ahadi kutoka utumwani Misri, njiani jangwani walitamani kula nyama. Badala ya KUSHUKURU na KUOMBA MUNGU awape nyama, wao walimnung’unikia MUNGU hata kunena vibaya mbele zake wakisema heri warudi Misri kwa masufuria ya nyama, pilau na vitunguu saumu. MUNGU akawakasirikia akawapa nyama nyingi za kwale lakini kabla ya kula aliwaangamiza. Je wewe unatamani nini hata kumnung’unikia MUNGU?. Inatupasa TUTOKE katika hali tulio nayo, ya moyo uliotawaliwa na utu wa kale na kumrudia MUNGU ili Atufikishe pale ALIPOTUKUSUDIA.''


Comments