MANENO YENYE HEKIMA NA UFAHAMU: (Mkalimani Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira).
''Hebu fuatia kisa cha mmoja wa Mitume wa BWANA YESU. Yuda Iskariote, alikuwa mmoja wa mitume 12 wa awali ambao BWANA YESU aliwateua miongoni mwa wengi Waliomfuata. BWANA YESU, Alijitenga ili Aombe kwa MUNGU usiku kucha peke yake ndipo Alipofanya Uteuzi wao. Bila shaka alifanya hivyo ili apate Hekima ya kuchagua watu walio sahihi. (Luka 6:12-16). Tena Yuda Iskariote, alipewa kutunza hazina ya Huduma, ikimaanisha kuwa alihakikishwa katikati ya wengi walioteuliwa. Baada ya mafunzo ya Huduma ya BWANA YESU, Mitume hawa walihitimu na kutumwa peke yao kwenda kuhudumia watu Dhidi ya mapepo wote, maradhi yote, na Kutangaza Ufalme wa MUNGU. Yuda alikuwa mmoja wao, ikimaanisha kuwa alikuwa na Sifa zilizotakiwa (Luka 9:1-6) (Inawezekana kabisa kuwa YESU Alijua fika Yuda alikuwa na MOYO MBAYA lakini Alimchagua ili ATUFUNDISHE JAMBO Fulani).
BWANA YESU na Mitume walivyoendelea na Huduma, yalizuka maswali ya faida gani watapata kwa kumfuata YESU na Huduma yake, hasa kwa kuwa wameacha vyote kwa ajili yake. Hapa inamaanisha mitume walitoa na kuacha vyote kwa ajili ya Huduma na Hawakuwa na chao tena bali vyote vilikuwa ni vya Shirika. Hapo BWANA YESU Alitoa masharti ya anayetaka kumfuata, kuwa ni lazima ajikane mwenyewe na abebe msalaba wake kila siku. Tena akaendelea kutahadharisha juu ya watu wanaongalia nyuma, kuwa hawafai kwa Ufalme wa MUNGU, (Luka 9:23-27,62). Akasisitiza juu ya mtu anayetaka kumfuata ahesabu Gharama kabla ya kuanza kazi (Luka 14:25-35, 18:18-30). Yuda ALIKUWEPO Anasikia.
Pamoja na Heshima yote hii, bado MOYO WA YUDA Ulikuwa SIYO MWAMINIFU wala MTAKATIFU, Kwa sababu, Alifikia mahali pa kuonyesha wazi Hila yake. Alijifanya ana Uchungu na Maskini, ALIPOONA Kiongozi wa Huduma BWANA YESU, ANAPAKWA MARHAMU YA BEI KUBWA. “YESU Alipopakwa marhamu ya nardo safi, Yuda Alihoji kwa nini Isiuzwe ili Fedha yake Wapewe maskini, si kwa KUWAHURUMIA bali kwa kuwa ni Mwivi, na ndiye Mshika Mfuko wa Huduma Akivichukua Vilivyomo humo” (Yohana 12:3-6). Ukosefu wa Uaminifu ULITHIBITISHWA baada ya Kifo chake, kwani ALIKWENDA KUJINYONGA katika Konde ALILONUNUA kwa Ijara ya Udhalimu; wakati Akiwa katika Utumishi. Tunasoma “Alianguka kwa kasi akapasuka matumbo yake yote yakatoka” (Matendo 1:18)''.
(NENO Hili litaendelea....)
Comments
Post a Comment