MANENO YENYE HEKIMA NA UFAHAMU

MANENO YENYE HEKIMA NA UFAHAMU: (Mkalimani Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira).

''MUNGU Anasema, “Wenye Haki wana mateso mengi”! Watu watasema, mbona huyu ana shida sana, mbona yuko hivi na hivi….waambie ni kweli maana wenye haki wana mateso mengi! Wayahudi ni watoto wake MUNGU, na MUNGU Alimwambia Ibrahim Atambariki na Watoto wake wote lakini wakawa Watumwa katika Nchi ya Misri. Wakamlilia MUNGU katika shida zao, katika maangamizo yao Wakamlilia BWANA kwa miaka 400 na BWANA AKAWAOKOA.

“Usione nina mateso mengi, yupo ANAYEKUJA KUNIOKOA”!

N.B. Kutoka Kanisa kwenda Kanisa, kwenda mikutano mbalimbali ya maombi HAIWEZI Kukutoa kwenye Matatizo mpaka UTAKAPOAMUA KUTOKA KWENYE TATIZO, Mpaka UTAKAPOAMUA na KUAMINI na KUKUBALI KWAMBA HAKI yako INATOKA kwa MUNGU na UNAIPATA kwa Sababu YESU KRISTO AMEKUFA KWA AJILI YAKO na AMELIPA DENI ZAKO ZOTE (Hapo ndipo UTATOKA KWENYE TATIZO).

Lakini bila ya kuelewa hivyo, utazunguka Makanisa mengi na Utaombewa na hilo tatizo Halitatoka mpaka utakapotambua Haki hiyo utaipataje na hayo mateso yamekujaje na yanaondolewaje.

(Maneno haya Matakatifu, Makuu Yenye HEKIMA na UFAHAMU Yataendelea)
Mwana wa MUNGU huu ni wakati wako wa KUTOKA, USIKUBALI Tena, Ni wakati wako Mwana wa MUNGU KUTOKA, ni wakati WAKO.
BWANA Akakuridhie.”

Comments

Popular posts from this blog

Mithali 8:17-21 "Nawapenda wale wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidii wataniona. Utajiri na heshima ziko kwangu, Naam, utajiri udumuo, na haki pia. Matunda yangu hupita dhahabu, naam, dhahabu safi, na faida yangu hupita fedha iliyo teule. Natembea katika njia ya haki, katikati ya mapito ya hukumu. Niwarithishe mali wale wanipendao, tena nipate kuzijaza hazina zao." Proverbs 8: 17-21 "I love them that love me; and those that seek me early shall find me. Riches and honour are with me; yea, durable riches and righteousness. My fruit is better than gold, yea, than fine gold; and my revenue than choice silver. I lead in the way of righteousness, in the midst of the paths of judgment: That I may cause those that love me to inherit substance; and I will fill their treasures."