Posts
Showing posts from January, 2014
Ni MWAKA WA KIBALI, MUNGU Atawawezesha, Atawasaidia, haijalishi umezaliwa vipi, Huu ni MWAKA WA KIBALI. Kichwa ni Mume, Wakina mama HESHIMU kichwa chako, Husipoheshimu kichwa chako, Mapato yako yatakosa Ulinzi, na MUNGU Akiona unaheshimu KICHWA CHAKO, ATAWEKA ULINZI Kwenye mapato yako. : Apostle & Prophet Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.
- Get link
- X
- Other Apps
ZONE ZONE ZONE: Leo ni Ibada katika Zone, Ibada katika Maeneo tunayoishi, Usikose Mwana wa MUNGU kuhudhuria, Ibada kwenye Zone kuna UPONYAJI, kuna kuwekwa HURU, kuna BARAKA za Uwinguni Haleluya,... Malaika wa BWANA Utembelea huko, kwa hiyo Usije ukapitwa, ...Mbarikiwe.
- Get link
- X
- Other Apps
DARASA/KONA YA MAFUNDISHO: ''Mkalimani Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY. (Darasa linaendelea pale lilipoishia jana,...) Yohana 8:32 “Tena mtaifahamu kweli nayo hiyo kweli itawaweka huru”. Unapofahamu ukweli wa jambo unapata Uponyaji, Ufumbuzi. Ni mambo mengi yamekusibu na yamekutesa na kukukandamiza kwa muda mrefu; ni vizuri ufahamu sasa kiini cha tatizo, kiini cha jambo ili ufikie mahali pa kutambua na kupona. Unapoenda hospitali hata kama umezidiwa sana, wanaweza wakakuwekea dripu za maji au dawa za kupunguza maumivu wakilenga kukusaidia upate muda kidogo ili waweze kutambua kiini cha tatizo; baadae watachukua vipimo labda damu, choo, mkojo, n.k na wakishagundua tatizo ni nini basi inakuwa rahisi kushughulikia hilo tatizo basi na huo unakuwa ndio uponyaji wako. Tatizo lisipogundulika,unaweza ukafa mapema. Kwa nini watu wa UKIMWI wanakufa mapema? Kwa sababu hawajatambua tatizo ni nini, wanaona tu matokeo yanayotokea mwilini na hatimaye kufa.; lakini malaria wameweza kuyashinda kwa sababu wametambua kiini chake ni mbu; na wale wadudu wanaosababisha wanawashughulikia kwa kuwaua na kuwapa wagonjwa dawa za kumaliza wale wadudu kulingana na wingi na aina zao. Mwanzo 3: 17-19 “Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako, michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni; kwa jasho la uso wako utakula chakula hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa, kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi. Ujumbe huu unatupatia kujua mwanzo au asili ya laana ni dhambi yaani kutosikiliza maagizo ya BWANA MUNGU WETU.
- Get link
- X
- Other Apps
Kufukuza pepo sio ujanja, Ujanja ni KULIJUA NENO. Unapomjua MUNGU unaponyeka magonjwa yote, Unachohitaji ni kuwa katika hali ya UTAUWA, UTAKATIFU. Huitaji kupanga foleni, Mjue SANA MUNGU, MPENDE SANA MUNGU, JUA NENO LAKE LINASEMA NINI, Mtumikie MUNGU, MUABUDU MUNGU, Ishi kama MUNGU Anavyosema, Husiishi kwa akili zako na kutazama Mazingira, Jua NENO, MPENDE SANA MUNGU. : Apostle & Prophet Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.
- Get link
- X
- Other Apps
KIBALI: Kuwepo kwetu Duniani ni KIBALI toka kwa MUNGU. Kuzaliwa kwako kwa kupitia tumbo la huyo Mama na kiuno cha huyo Baba ni KIBALI. MUNGU ALIWARIDHIA wao wakuzae Wewe, kwa njia gani, kwa namna gani MUNGU Anajua. Ulizaliwaje liwaje ISIKUSUMBUE, kwamba walikuwa na Dini, Imani MUNGU Aliwaridhia, MBEGU ilitoka ikaingia ukatokea. Kuna watu wanafanya uasherati toka asubuhi hadi usiku, wengine wameoana na watakatifu lakini hawajapata Mtoto; Ila Wewe ULIZALIWA,....: Apostle & Prophet Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY, sehemu ya Mahubiri ya Jumapili jana tarehe 26/Jan/2014; (Mahubiri kamili yatapatikana kwenye Website yetu www.efathaministry.org, na kwenye Youtube yetu www.youtube.com/efathaministry pamoja na kwenye Blog yetu www.efathaministrypage.blogspot.com, Mbarikiwe wana wa MUNGU).
- Get link
- X
- Other Apps
Watoto wakiwa mbele za bwana tayari kwa ibada ya asubuhi Tarehe 26 January 2014,Waacheni watoto waje kwangu, Maana watauridhi Ufalme wa Mbinguni! Amen
- Get link
- X
- Other Apps
Biblia inasema usiende mikono mitupu nyumbani mwa Bwana, watumishi wa Mungu wakitoa sadaka wakiongozwa na Mtume na Nabii Josephat Eliasi Mwingira .
- Get link
- X
- Other Apps
SHUHUDA ZA JUMAPILI YA TAREHE 26th JANUARY 2014 Mungu wetu ni mkuu sana, Mungu wetu ametukubali kwani tumepata kibali na watumishi wa Mungu kama wanavyo onekana mioyo yao inashukrani na wengi wao wamepata watoto wengine watoto wao walikuwa wanaumwa tangu kuzaliwa kwao lakini sasa hivi wana moyo wa shukrani Binti yao anatembea pia kuna Mtumishi wa Mungu anamshukuru Mungu kwani anamiaka 10 ya wokovu miaka 7 ya utumishi na miaka 6 ya ndoa hawana zaidi ya kumpatia Mungu zaidi ya Kumshukuru Mungu. “Mungu hana Upendeleo” Mungu hajakuacha na wewe msongeree naye atakupa KIBALI AMIN!!
- Get link
- X
- Other Apps
Moyo wangu umeamua kukutumikia wewee! Moyo wangu umeamua kukutumikia wewee!! Tumutumikie mungu wetu kwa mioyo yetu kwa sababu (Mwenye HITIMISHO la Maisha yako sio boss wako au ndugu yako, ni MUNGU. : Apostle & Prophet Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY)
- Get link
- X
- Other Apps
Mwenye HITIMISHO la Maisha yako sio boss wako au ndugu yako, ni MUNGU. : Apostle & Prophet Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY
- Get link
- X
- Other Apps
Leo ni Siku ya kwenda zone, kumuambudu mungu wetu twende na familia zetu, njoo na kondoo mungu akubariki sana kwa utii wako!
- Get link
- X
- Other Apps
Kelele haiji ulizaliwa vipi, inakuja unamalizia vipi Safari yako ya kuishi. Kwamba baba yako anaitwa nani haikusaidii. Vyovyote ulivyozaliwa isikusumbue (kwamba mama yako alibakwa, alidanganywa, chipsi zilizasababisha, lifti ilisababisha, iwe stendi ya basi n.k., vyote visikusumbue), la msingi angalia jinsi gani UNAVYOSONGA MBELE. Hakuna hata mmoja atakayetaka azaliwe na nani. BABA wa Mbinguni ndiye Asili ya kuzaliwa kwetu. ASILI yako wewe ni MUNGU, ndio maana wewe ni MALI YA MUNGU.: Apostle & Prophet Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.
- Get link
- X
- Other Apps
Haijalishi Umezaliwa katika Mazingira gani, maadamu Wewe UMEOKOKA, UMEMKUBALI YESU KRISTO kuwa BWANA na MWOKOZI wa Maisha yako, ..... MSIKIE Mama huyu na Mwanae: Kipindi huduma hii ya MUNGU Wetu MKUU EFATHA MINISTRY inaanza pale Sinza, huyu mama alikuwa anatembea na kandambili tena zimechoka huku akiwa hoi taabani kimaisha akiuza MCHICHA Mchicha mitaani. Mtumishi wa MUNGU Mbeba Kusudi Mkalimani wetu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira alikutana naye, naye Mama AKAMPOKEA YESU KRISTO Awe BWANA na MWOKOZI wa Maisha yake, baada ya Kuokoka akawa Anaendelea na Biashara yake ya Mchicha Mchicha, Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Akawa anamwombea, akawa anamwombea Mchicha UISHE Haraka ili awe anakuja kwenye MAOMBI, Na KWELI ilikuwa haichukui muda Mchicha mtaa wa kwanza, wa Pili UMEISHA, Hakuwa anachukua muda tena kutembea JUANI kwani Mchicha ulikuwa unamalizika mara moja kwa haraka sana. Mama huyu akawa anaendelea na Biashara yake LAKINI Sasa Akafikia wakati akawa na Vijana WANAMLIMIA na Yeye anaenda kuuza tu, Haleluyaaa...., SASA LEO HII Mwanae huyu (Pichani) AMEMALIZA ELIMU ya Chuo KIkuu''DEGREE''. Yule yule Mama Mchicha Mchicha aliyekuwa anatembea Juani, kandambili zimechoka, Maisha magumu taabani LEO SI YEYE TENA na MWANAE ANA DEGREE...Ndipo UONE Jinsi Gani MUNGU WETU ALIVYO MZURI, Uone jinsi gani YESU ALIVYO MZURIIII, Unataka Nini TENA? MWAMINI YESU, MPOKEE YESU, TULIA KWA MKALIMANI WAKO na MSIKILIZE VIZURI na ELEWA ANAKUAMBIA NINI... EFATHA ''FUNGUKA''. Ooooooh Haleluyaaaaaa Asante YESU, Asante YESU, Asante YESU, Tunakupenda BWANA, Tunakupenda YESUUU, Wewe ni MZURI YESU, Wewe ni MZURI, UNATUPENDA Wanao, Asante Nasi TUNAKUPENDA.
- Get link
- X
- Other Apps
Haleluya... UTUKUFU na SIFA ni Kwa BWANA MUNGU Wetu MKUU, Tunamwambia BWANA Asante, MUNGU Wetu MKUU Asante, Ibada ya kwanza ndio imemalizika, Uwepo wa BABA MUNGU Wetu Ulionekana ukitawala,... ''Ni PENDO LA NAMNA GANI ALILOTUPA BABA...", Ooooh Haleluyaaaaaaa ''NIMEPAKWA MAFUTA, Nimepakwa Mafutaaaaaaaa'' Kila kitu ni "FULL MASSIVE IN ORDER''
- Get link
- X
- Other Apps
SHUHUDA SHUHUDA SHUHUDA: ASTELIA CHILAMBO, ZONE YA MBEZI BEACH B’ Anamshukuru MUNGU kwa kumponya mateso ambayo alikuwa anayapata kwa kuumwa mara kwa mara, kwa muda mrefu alikuwa akiteseka kwa magonjwa alikuwa akienda shuleni mama yake alikuwa anapigiwa simu kuwa mwanae anaumwa, mara nyingine ata usiku wa manane, mateso haya yalikuwa ni kawaida kwake toka baba yake alipofariki mwka 2007 (Wanasema baba yake alikuwa anampenda sana). Jumapili moja alikuja Kanisani Ibadani, akapata Neema ya kukutana na Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii, Mtumishi wa MUNGU akamwambia achemshe maziwa na anywe kwani alikuwa hanywi maziwa kutokana na vidonda vya tumbo, akanywa maziwa, baada ya hapo Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii alimpa maji na kumuambia anywe kidogo kidogo, HALELUYA UTUKUFU KWA MUNGU WETU JUU, toka hapo akawa amepona kabisa. Baada ya hapo alirudi shuleni lakini akawa anawaza sana kuhusu Mitihani kwani kabla ya Kuombewa na Mtumishi wa MUNGU alikuwa ana kipindi hajahudhuria masomo shuleni, kwa hiyo alikuwa anawaza kuhusu atafanyaje mitihani, lakini akamuomba MUNGU somo la Chemistry aweze kufaulu, HALELUYA MUNGU WETU NI MZURI, MUNGU wetu Alifanya Matendo yake MAKUU Astelia akawa wa kwanza katika Shule zote walizo kuwa wakishindanishwa katika hilo Somo la Chemistry. HALELUYA sasa Astelia Ni MZIMA wa Afya Njema na Anafanya VIZURI katika Masomo yake, SIFA KWA BWANA WETU YESU KRISTO ALIYE HAI ALFA na OMEGA, Asante YESU BWANA kwa KUTUPENDA SANA na Ukatupa KUSUDI HILI (EFATHA: Uponyaji na Ukombozi, Watu WAWEKWE HURU), Asante YESU, Tunakupenda BWANA, Asante. (Na Wewe uko unayeteseka, Jua KWAMBA YESU Anakupenda sana, YESU Anakuambia NJOO SASA, Naye ATAKUWEKA HURU, ANAKUPENDA, Njoo kwa YESU)
- Get link
- X
- Other Apps
In God’s Presence - A Night of Holy Praising Service. Psalms 37:4 - We delight ourselves in the Lord, and ensure His Presence with us to grant desires of our hearts. What’s your desire?! Come and Experience heavens down with you. On January 17 2014 . Efatha Ministry –Mwenge Premises, 21:00 HRS to dawn.
- Get link
- X
- Other Apps
MIUJIZA ni kwa ajili ya WASIOOKOKA (ili wakiona WAAMINI MUNGU YUPO), na NENO ni kwa ajili ya WALIOOKOKA maana wanapata Chakula cha kuwatia AFYA na NGUVU ya KUMKIMBIZA shetani, Waliookoka waana KIBALI cha Kumkimbiza shetani.: Apostle & Prophet Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.
- Get link
- X
- Other Apps
Huu ni Mwaka wa KIBALI 2014: Kila kitu kitazidishwa MARA TATU (x 3 Times) Unaenda KUPOKEA;... kama ni Kipato x 3, Cheo x 3, Biashara x 3, Afya Njema x 3, Ustawi x 3, Mshahara x 3, Unachokipanga x 3, (na ....)... You are going to receive TRIPLES....: Apostle & Prophet Josephat Elias Mwingira (Baraka zilizoachiliwa jana kutoka Madhabahuni)
- Get link
- X
- Other Apps
Haleluya,... YESU Wetu Ni MZURI, MUNGU Wetu ni MZURI, Tunamshukuru MUNGU Wetu MKUU jana tuliopokea Baraka ya Mtoto, Mtoto alizaliwa nyumbani Hemani Mwa BWANA Kanisani EFATHA MINISTRY Mwenge Dar es Salaam, Tanzania. Mtoto alikuwa na kilo 3, Mama wa Mtoto Whitness Temu wa eneo la Sayuni, Mtoto alizaliwa salama salmini,... Haleluyaaa SIFA KWA YESU BWANA WETU, Efatha....Fungukaa,... MWAKA WA KIBALI, Hakuna kitakachowazuia WANA WA MUNGU WANA EFATHA, HAKUNA.
- Get link
- X
- Other Apps
''UFAHAMU ni kwa UTUKUFU WA MUNGU, na Ukipata Ufahamu ni rahisi kuponyeka. Maombi sio kwamba ndio yatakufanya Kupokea, BALI NI UELEWA WAKO, UMEELEWA NINI WEWE. Maombi ya Mtu mwenye UFAHAMU ni Mafuta, Ni Manukato kwa MUNGU.'' : Apostle & Prophet Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY (Baadhi ya Nukuu za Mahubiri ya jana Ibadani Tarehe 05/January/2014)
- Get link
- X
- Other Apps
Mtumishi wa MUNGU Mbeba KUSUDI Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira wakati akitoa Salamu za MWAKA MPYA 2014...!
- Get link
- X
- Other Apps