DARASA/KONA YA MAFUNDISHO: ''Mkalimani Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY. (Darasa linaendelea pale lilipoishia jana,...) Yohana 8:32 “Tena mtaifahamu kweli nayo hiyo kweli itawaweka huru”. Unapofahamu ukweli wa jambo unapata Uponyaji, Ufumbuzi. Ni mambo mengi yamekusibu na yamekutesa na kukukandamiza kwa muda mrefu; ni vizuri ufahamu sasa kiini cha tatizo, kiini cha jambo ili ufikie mahali pa kutambua na kupona. Unapoenda hospitali hata kama umezidiwa sana, wanaweza wakakuwekea dripu za maji au dawa za kupunguza maumivu wakilenga kukusaidia upate muda kidogo ili waweze kutambua kiini cha tatizo; baadae watachukua vipimo labda damu, choo, mkojo, n.k na wakishagundua tatizo ni nini basi inakuwa rahisi kushughulikia hilo tatizo basi na huo unakuwa ndio uponyaji wako. Tatizo lisipogundulika,unaweza ukafa mapema. Kwa nini watu wa UKIMWI wanakufa mapema? Kwa sababu hawajatambua tatizo ni nini, wanaona tu matokeo yanayotokea mwilini na hatimaye kufa.; lakini malaria wameweza kuyashinda kwa sababu wametambua kiini chake ni mbu; na wale wadudu wanaosababisha wanawashughulikia kwa kuwaua na kuwapa wagonjwa dawa za kumaliza wale wadudu kulingana na wingi na aina zao. Mwanzo 3: 17-19 “Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako, michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni; kwa jasho la uso wako utakula chakula hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa, kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi. Ujumbe huu unatupatia kujua mwanzo au asili ya laana ni dhambi yaani kutosikiliza maagizo ya BWANA MUNGU WETU.

Comments