Posts
MCH. MICHAEL OLAWORE KUTOKA UK (Hapa Precious Center Kibaha).. Rumi 8:1 “Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.” Akili yako inaweza kutawaliwa, akili yako ikishikwa na Roho wa Mungu itakuwa salama lakini ikishikwa na ibilisi ni tatizo, ruhusu akili yako itawaliwe na Roho Mtakatifu itasababisha matokeo chanya. Kila kinachoshika akili yako kitaamua matokeo ya maisha yako. Mruhusu ROHO wa MUNGU aongoze akili yako Leo.
- Get link
- X
- Other Apps
MCH. MICHAEL OLAWORE KUTOKA UK (Hapa Precious Center Kibaha).. Rumi 8:1 “Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.” Akili yako inaweza kutawaliwa, akili yako ikishikwa na Roho wa Mungu itakuwa salama lakini ikishikwa na ibilisi ni tatizo, ruhusu akili yako itawaliwe na Roho Mtakatifu itasababisha matokeo chanya. Kila kinachoshika akili yako kitaamua matokeo ya maisha yako. Mruhusu ROHO wa MUNGU aongoze akili yako Leo.
- Get link
- X
- Other Apps
Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira: Amani ni ufunguo wa mafanikio na kama hauna amani sahau kufanikiwa hivyo amani ni jambo la muhimu sana katika maisha yako na inakutenga mbali na maadui. Amani inakupa afya kama hauna amani hata afya yako itakuwa mbaya, siku utakapopokea amani katika maisha yako ndipo mafanikio yako yataitika. Kukosa amani kunasababisha tatizo la kungoa meno na kuvaa miwani katika umri mdogo.
- Get link
- X
- Other Apps
Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira: Kazi za Roho wa Bwana juu yangu: 1. Kuhubiri injili, 2. Kuponya na kufanya miujiza, 3. Kufungua macho ya vipofu na kuwapa watu mafunuo, Mithali 8:17-20 “Nawapenda wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona. Utajiri na heshima ziko kwangu, .....” 4. Kuwekwa huru, huwezi kupata uhuru kama hujajua kweli na kweli tunaipata kupitia macho yetu, ukishawekwa huru ndipo unaweza kuomba, kama hujakombolewa au hujawekwa huru utakuwa hauabudu bali unalia tu. Ukombozi sio kumtoa mtu pepo bali ni kumwamisha mtu kutoka katika maisha aliyoyazoea. 5. Yuko ili akupe amani. Unapokuwa na vurugu mahali anakupa amani na usipokuwa na huyu Roho utaona vurugu kila mahali hata mtu anafika mahali anasema watu hawanipendi. Roho wa Bwana anapokuja kwa mtu kitu cha kwanza anampa amani.
- Get link
- X
- Other Apps
MTUME NA NABII JOSEPHAT E. MWINGIRA SOMO: Roho wa Bwana Juu yangu. Mungu anafikiri kufanya kitu Fulani ila humtumia mtu kukamilisha kile anachofikiria. Mtendaji ni mtu sio Mungu, Mungu anaachilia Nguvu ya kumuwezesha mtu kutenda jambo hilo alilolikusudia. Ndiyo maana akakuleta wewe duniani ili uweze kutimiza jambo fulani analohitaji lifanyike duniani. Ili uweze kutekeleza jambo lolote la Kiungu unahitaji ROHO WA BWANA. Huyu anakupa nguvu ya kukuwezesha kufanya jambo hilo. TAMANI kupokea NGUVU HII.
- Get link
- X
- Other Apps
PASTOR MICHAEL OLAWARE KUTOKA UK (KATIKA KUSANYIKO KUU 2016) SOMO : KUVUNJA KIZUIZI MBELE YAKO Ukivunja vizuizi itakurahisishia kufika mbali kwa sababu mbele ya kuvunja mipaka kuna Baraka zako ila usipo vunja utabaki hapo ulipo. Maisha ya kawaida ni tatizo hakuna mtu aliumba kuishi maisha ya kawaida bali kipo kizuizi kinacho kuzuilia kufika mahali ambapo Mungu amekukusudia. Vikwazo ni:- 1. Mazoea : Amua kutoka kwenye aina ya maisha uliyoyazoea 2. Maoni ya wanadamu: Acha kusikiliza kile watu wanasema juu yako, kwama huwezi hiki au kile 3. Wewe mwenyewe kuwa kikwazo: Kujiona huwezi, eti kwa kuwa hujasoma, au familia yenu haijaifanikiwa. UKITAKA KUFANIKIWA LAZIMA USHINDE HIVYO VIKWAZO
- Get link
- X
- Other Apps