IBADA YA KUFUNGA NA KUOMBA SIKU YA TISA: MTUMISHI: ADVESTA MLENGUS. Mungu anataka nini kwetu sisi TULIOITWA na KUTEULIWA ili tuzae MATUNDA? Isaya 42:6-7 “Mimi, Bwana, nimekuita katika haki, nami nitakushika mkono, na kukulinda, na kukutoa uwe agano la watu, na nuru ya mataifa; kuyafunua macho ya vipofu, kuwatoa gerezani waliofungwa, kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa.” Mungu amekuita katika haki yake maana wewe ni haki yake na atakushika mkono wako ili usipotee. Mungu AMEKURIDHIA wewe uwe AGANO LA WATU, Yeye anafanya AGANO na WEWE ili na wewe ukafanye agano na watu wake. Kama vile alivyo fanya agano na Musa la kuwakomboa wana wa Israel. Mungu amefanya agano na wewe ili uwe NURU ya MATAIFA ili kwa hiyo Nuru ukafunue macho ya watu ambao wana macho lakini hawaoni na wenye masikio lakini hawasikii, uwatoe watu walio katika hali ya kufungwa. Hili ni agano lako na Mungu, yaani amekuita na katika kukuita amekuweka katika haki yake. Mung...
Posts
Showing posts from May, 2017
- Get link
- X
- Other Apps
KAA mbali na DHAMBI, ukitenda Mema, ukitenda MATAKATIFU dhambi inakaa mbali na Wewe, lakini ukitenda ya Maovu, dhambi inakunyemelea, Uharibifu unakusogelea. Mwana wa MUNGU ACHA KUWAZA MABAYA, wala USIJIWAZIE Mabaya, MUNGU Awe wa Kwanza kwa Kuwaza yale yaliyo MAZURI katika Mawazo yako. Mithali 8:17-21 “Nawapenda wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona. Utajiri na Heshima ziko kwangu, Naam, Utajiri udumuo, na haki pia. Matunda yangu hupita dhahabu, naam, dhaha bu safi, Na faida yangu hupita fedha iliyo teule. Natembea katika njia ya haki, Katikati ya mapito ya hukumu. Niwarithishe mali wale wanipendao, Tena nipate kuzijaza hazina zao.” HAKUNA,…. MUNGU Akikubariki leo kesho Aache kukubariki, HAKUNA…..MUNGU Akikubariki basi ndivyo itakavyokuwa INAENDELEA, lakini lazima UMPENDE, lazima UISHI MAISHA YATAKAYOMPENDEZA MUNGU, lazima UISHI Maisha MATAKATIFU, Dhambi Ikae mbali na Wewe. - Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.
- Get link
- X
- Other Apps
IBADA EFATHA MINISTRY MWENGE DAR ES SALAAM: MTUME NA NABII JOSEPHATI ELIAS MWINGIRA. Mambo MAWILI yanayoweza KUMFURAHISHA MUNGU ni:- • (1) Moyo wa SHUKRANI. • (2) Moyo wa KUMTAFUTA Mungu na KUTAFUTA MTU Mmoja ili AMJUE Mungu. Ukifanya haya Mambo MAWILI kwa SHUKRANI na kwa BIDII naamini kwa MOYO wangu wote hatakama ulikuwa huoni njia katika Maisha yako Mungu ATAKUFUNGUA macho. Mungu Anapenda MTU mwenye Moyo wa SHUKRANI, Mshukuru YEYE Mwambie Asante kwa Miguu maaana wako watu ambao hawana miguu, mwambie ASANTE kwa sababu wengine wako mochwari lakini Wewe amekupa AFYA Njema. Safari hii tuna ajenda moja tu ya KUTAFUTA wale Wasiomjua Mungu ili WAZIACHE Njia wanazoziendea na WAMRUDIE Mungu, Utakapo mpata huyo MTU hakikisha ANAKUWA Kiroho kama Wewe. Mungu hadhihakiwi, kile utakacho fanya ndicho kitakachokuwa. Mungu HATANIWI, na hicho Unachokifanya ndicho kitakachokuwa. AMUA Kubadilika na KUACHA yale Yasiyompendeza Mungu na fanya ili MUNGU Aakufurahie.
- Get link
- X
- Other Apps
MAMA ELIAKUNDA MWINGIRA: MUNGU wetu ni Mungu wa Mpangilio na Mwaminifu, Mungu ana Mpango na wewe, haijalishi unapitia magumu gani LEO unapaswa kujua Mungu AMEKUSIKIA kilio chako. Yumkini umefika mahali umekuwa mbali na YEYE ni kwa sababu ulifanya Maovu ambayo yamekupeleka uwe kwenye mateso. Maisha ya uovu ndiyo yanayokupelekea uingie kwenye Maumivu. Ishi Maisha ya KUMPENDEZA Mungu ili Umfurahishe YEYE ili Akutoe kwenye Maumivu na Mateso unayopitia. Huu ni Mwezi wa Maombi, unatakiwa kutembea katika UTAKATIFU ili Umuone Mungu, zingatia wakati huu tuliopewa kwa KUJINYENYEKEZA mbele Zake ili Akuondolee hayo Mateso na Magumu unayopitia, ukitembea katika UTAKATIFU Mwezi huu Hautapita bure bali YEYE ATAKUONDOLEA Maumivu na Mateso unayoyapitia. MUNGU wetu ni Mungu wa REHEMA, YEYE Anasamehe maana hata mchawi anayewanga Akitubu Mungu anasamehe. Mtu wa Mungu geuka, ACHA Dhambi na Kuishi Maisha ya KUZOELEA dhambi. ROHO MTAKATIFU ndiye Anayetupa KUTUBU na KUTENGENEZA lakini ukimtia kisi...
- Get link
- X
- Other Apps
IBADA YA KUFUNGA NA KUOMBA SIKU YA NANE: MTUMISHI: ADVESTA MLENGUS. Yohana 15:16 “ Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni. ” Bwana YESU alituombea kwa BABA ili tulindwe na Yule mwovu kwa sababu alikuwa anajua kuwa AMETUCHAGUA na KUTUWEKA ili tufanye KAZI YAKE. Si wewe uliyejichagua na kujiweka hapo ulipo na kwenye nafasi uliyonayo bali ni YEYE aliyekuchaguwa. Mungu hawezi kukupa kitu ambacho hukiwezi kukifanya, wewe uliye Kiongozi fahamu kuwa Alikuchagua kabla ya kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu. Tunapaswa kuwaheshimu Viongozi waliowekwa mbele yetu, Mchungaji, Askofu Kiongozi wa cell n.k, kwa maana wao hawakujichagua bali ni Bwana YESU. Ukijua kuwa kiongozi wako aliwekwa na nani katika nafasi aliyoko Utamuheshimu. Mathayo 22:14 “ Kwa maana waitwao ni wengi, bali wateule ni wachache.” Usikae katika nafasi ya kuitwa bali kaa ka...
- Get link
- X
- Other Apps
IBADA YA KUFUNGA NA KUOMBA SIKU YA NANE: MTUMISHI: ADVESTA MLENGUS ZABURI 75:1 “Ee Mungu, twakushukuru. Twakushukuru kwa kuwa Jina lako li karibu; Watu huyasimulia matendo yako ya ajabu.” Unapaswa KUMSHUKURU Mungu kwa kila kitu alichokupa katika Maisha yako, MSHUKURU kwa Pumzi aliyokupa maana pasipo YEYE huwezi Kuishi, YEYE ni chanzo cha UHAI na UZIMA wako. Mungu anafurahia MOYO wa SHUKRANI hivyo ili UMPENDEZE inakupasa uwe na Moyo wa SHUKRANI mbele zake. Muombe Mungu akupe NGUVU yake ili uweze Kutenda yale aliyokupa katika UBORA, UHODARI na USHUJAA pasipo Woga wowote, maana bila NGUVU yake huwezi Kufanya kitu chochote. Hiyo NGUVU ikikushukia inakupa kufanya Mambo yako kwa URAHISI na WEPESI zaidi. Wafilipi 4:13 “Nayaweza mambo yote katika YEYE anitiaye Nguvu. ”