MAMA ELIAKUNDA MWINGIRA:
MUNGU wetu ni Mungu wa Mpangilio na Mwaminifu, Mungu ana Mpango na wewe, haijalishi unapitia magumu gani LEO unapaswa kujua Mungu AMEKUSIKIA kilio chako.
MUNGU wetu ni Mungu wa Mpangilio na Mwaminifu, Mungu ana Mpango na wewe, haijalishi unapitia magumu gani LEO unapaswa kujua Mungu AMEKUSIKIA kilio chako.
Yumkini umefika mahali umekuwa mbali na YEYE ni kwa sababu ulifanya Maovu ambayo yamekupeleka uwe kwenye mateso. Maisha ya uovu ndiyo yanayokupelekea uingie kwenye Maumivu.
Ishi Maisha ya KUMPENDEZA Mungu ili Umfurahishe YEYE ili Akutoe kwenye Maumivu na Mateso unayopitia.
Huu ni Mwezi wa Maombi, unatakiwa kutembea katika UTAKATIFU ili Umuone Mungu, zingatia wakati huu tuliopewa kwa KUJINYENYEKEZA mbele Zake ili Akuondolee hayo Mateso na Magumu unayopitia, ukitembea katika UTAKATIFU Mwezi huu Hautapita bure bali YEYE ATAKUONDOLEA Maumivu na Mateso unayoyapitia.
MUNGU wetu ni Mungu wa REHEMA, YEYE Anasamehe maana hata mchawi anayewanga Akitubu Mungu anasamehe. Mtu wa Mungu geuka, ACHA Dhambi na Kuishi Maisha ya KUZOELEA dhambi. ROHO MTAKATIFU ndiye Anayetupa KUTUBU na KUTENGENEZA lakini ukimtia kisirani Anaondoka na Anakuacha.
Wewe ULIYEOKOKA ACHA Dhambi, unayesema Bwana YESU Asifiwe lakini ni MDOMONI tuu wakati Moyo umeuelekeza mahali pengine kwenye uongo, usengenyaji, au kwa mke mdogo hiyo ni DHAMBI. Moyo una ugonjwa wa Kufisha, BADILISHA Tabia yako.
Ukimpata ROHO MTAKATIFU Atakupa dira wapi unatakiwa uende, Akiingilia Maisha yako ATAKUBADILISHA.
Kipindi hiki cha Maombi Atakubadilisha Usiangalie Mazingira, Usitegemee Akili zako wala Usimtegemee mtu maana imeandikwa kuwa "Yeyote amtegemeaye mwanadamu amelaaniwa", MUAMINI na UMTEGEMEE YEYE TU naye Atabadilisha Maisha yako nawe utakuwa BORA kati ya Walio BORA.
Comments
Post a Comment