IBADA YA KUFUNGA NA KUOMBA SIKU YA NANE:
MTUMISHI: ADVESTA MLENGUS

ZABURI 75:1 “Ee Mungu, twakushukuru. Twakushukuru kwa kuwa Jina lako li karibu; Watu huyasimulia matendo yako ya ajabu.”
Unapaswa KUMSHUKURU Mungu kwa kila kitu alichokupa katika Maisha yako, MSHUKURU kwa Pumzi aliyokupa maana pasipo YEYE huwezi Kuishi, YEYE ni chanzo cha UHAI na UZIMA wako. Mungu anafurahia MOYO wa SHUKRANI hivyo ili UMPENDEZE inakupasa uwe na Moyo wa SHUKRANI mbele zake.
Muombe Mungu akupe NGUVU yake ili uweze Kutenda yale aliyokupa katika UBORA, UHODARI na USHUJAA pasipo Woga wowote, maana bila NGUVU yake huwezi Kufanya kitu chochote. Hiyo NGUVU ikikushukia inakupa kufanya Mambo yako kwa URAHISI na WEPESI zaidi. Wafilipi 4:13 “Nayaweza mambo yote katika YEYE anitiaye Nguvu. ”

Comments