IBADA YA KUFUNGA NA KUOMBA SIKU YA TISA:
MTUMISHI: ADVESTA MLENGUS.
Mungu anataka nini kwetu sisi TULIOITWA na KUTEULIWA ili tuzae MATUNDA?
Isaya 42:6-7 “Mimi, Bwana, nimekuita katika haki, nami nitakushika mkono, na kukulinda, na kukutoa uwe agano la watu, na nuru ya mataifa; kuyafunua macho ya vipofu, kuwatoa gerezani waliofungwa, kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa.”
Mungu amekuita katika haki yake maana wewe ni haki yake na atakushika mkono wako ili usipotee. Mungu AMEKURIDHIA wewe uwe AGANO LA WATU, Yeye anafanya AGANO na WEWE ili na wewe ukafanye agano na watu wake. Kama vile alivyo fanya agano na Musa la kuwakomboa wana wa Israel.

Mungu amefanya agano na wewe ili uwe NURU ya MATAIFA ili kwa hiyo Nuru ukafunue macho ya watu ambao wana macho lakini hawaoni na wenye masikio lakini hawasikii, uwatoe watu walio katika hali ya kufungwa. Hili ni agano lako na Mungu, yaani amekuita na katika kukuita amekuweka katika haki yake.
Mungu amekuamini wewe ili uwe agano na hao mataifa ambao wametekwa na kuwekwa gerezani ili uwatoe na kuwaweka nuruni, aliyekuwa gerezani hawezi kuona kitu chochote ni mpaka awe nuruni.
Mungu amekuamini wewe ili uwe agano na hao mataifa ambao wametekwa na kuwekwa gerezani ili uwatoe na kuwaweka nuruni, aliyekuwa gerezani hawezi kuona kitu chochote ni mpaka awe nuruni.
Comments
Post a Comment