IBADA YA KUFUNGA NA KUOMBA SIKU YA NANE:
MTUMISHI: ADVESTA MLENGUS.
Yohana 15:16 “Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni.
Bwana YESU alituombea kwa BABA ili tulindwe na Yule mwovu kwa sababu alikuwa anajua kuwa AMETUCHAGUA na KUTUWEKA ili tufanye KAZI YAKE. Si wewe uliyejichagua na kujiweka hapo ulipo na kwenye nafasi uliyonayo bali ni YEYE aliyekuchaguwa. Mungu hawezi kukupa kitu ambacho hukiwezi kukifanya, wewe uliye Kiongozi fahamu kuwa Alikuchagua kabla ya kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu.
Tunapaswa kuwaheshimu Viongozi waliowekwa mbele yetu, Mchungaji, Askofu Kiongozi wa cell n.k, kwa maana wao hawakujichagua bali ni Bwana YESU. Ukijua kuwa kiongozi wako aliwekwa na nani katika nafasi aliyoko Utamuheshimu.
Mathayo 22:14 “Kwa maana waitwao ni wengi, bali wateule ni wachache.” Usikae katika nafasi ya kuitwa bali kaa katika nafasi ya kuteuliwa, ukikaa hapo Utamuheshimu aliye mbele yako yaani (Kiongozi wako). Unapaswa kumuheshimu na ukimuheshimu Yeye utakuwa ni sawa na Kumuheshimu yule aliyemuweka ambaye ni MUNGU.
Kiongozi usipoitunza nafasi yako na kukaa vizuri Mungu akikutoa hapo anamuweka mwingine, kubali kile ulichopewa ukitendee Kazi kwa UBORA, UHODARI na USHUJAA.
Mungu anawachukia watu Wavivu wale wanao tenda kazi kwa ULEGEVU.

Comments