Posts

Showing posts from September, 2016

MCHUNGAJI: MELENIA IRENGO SOMO: TABIA Tabia humtambulisha mtu katikati ya watu, tabia yako itakutambulisha kwa watu kuwa wewe ni wa namna gani. Tabia inaweza kumuinua mtu kutoka chini na kumketisha juu. Mfano Mfalme Daudi alikuwa na tabia nzuri tangu akiwa mdogo na Mungu akamuinua kutoka kuchunga kondoo wa Baba yake na kumfanya kuwa Mfalme, tabia nzuri ndiyo inaweza kusababisha ukainuliwa kutoka chini na kuwekwa juu na wafalme. Wagalatia 6:7 “Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.” Unatakiwa ujitathmini mwenyewe kwanza unapanda nini kwa Mungu au kwa watu ili usije ukavuna usicho kitegemea kwa kuwa ukipanda mazuri ndiyo utakayo vuna na pia ukipanda mabaya ndiyo utakayo vuna, panda mema kwa Mungu au watu ili uvune mema. Rumi 8:14 “Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.” ukitaka kutembea na tabia ya Mungu hakikisha unaongozwa na Roho wake maana ukiongozwa na Roho hutafanya yasiyo MPENDEZA MUNGU maana ROHO wa MUNGU ANAKUPA NEEMA jinsi ya kuenenda hapa chini ya jua.

Image

MCHUNGAJI: MELENIA IRENGO SOMO: TABIA Tabia ni nini? Tabia ni matendo, mienendo au sifa mbalimbali za mtu zinazoambatana na matendo yake au Nafsi yake. Tabia ziko za aina mbili:- 1. Tabia nzuri: Hii ni tabia inayotoka kwa Mungu. 2. Tabia mbaya: Hii ni Tabia inayotoka kwa ibilisi. Uwe na TABIA NZURI ili watu watamani kuwa kama wewe kwa sababu tabia nzuri INAVUTA watu karibu na wewe. Mfano mzuri ni BWANA wetu YESU KRISTO alikuwa na tabia ya KUWAVUTA WATU ILI WAMJUE MUNGU. Uwe na tabia ya kuwavuta watu ili wamjue Mungu na usiwe na tabia ya kuwakimbiza watu, iwe ni kwa maneno au kwa chochote kile mahali popote utakapokuwepo. Wagalatia 5:16-24 “Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.......”

Image

Karibu kwenye kusanyiko Kuu 2016 - efathaministry Mtume na Nabii Josephat E. Mwingira anayofuraha kubwa kuwakaribisha wote kwenye Kusanyiko Kuu la Efatha litakalofanyika kuanzia Tarehe 3 Oktoba 2016 hadi Tarehe 11 Oktoba 2016. Ni kambi ya wiki moja ambayo itaanza siku ya… EFATHAMINISTRY.ORG

Image
http://www.efathaministry.org/karibu-kwenye-kusanyiko-kuu-…/

MAMA ELIAKUNDA MWINGIRA: Usiangalie mazingira uliyonayo maana ukiangalia mazingira huta toka bali inua macho yako kwa Bwana na umtazame yeye tu maana yeye ndiye msaada wako na hata kuacha kamwe. Ndani ya Kristo Yesu kuna raha, jifunze kujitamkia mazuri maana kinywa chako kinaumba usiseme hawanipendi, maana jinsi ajionavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo. Je unajionaje wewe? Mnyonge, mbaya au hufai ? Mungu hata pingana na wewe. Mungu siyo Shangazi yako wala Mjomba wako Mungu ni Mungu tu na wala usimfananishe na Mwanadamu. kama Shangazi yako au Baba yako anakuchukia usimfananishe na Mungu, Mungu wetu ni Mungu wa Upendo anakuwazia mema kila iitwapo leo.

MCHUNGAJI DAVID URIO. SOMO:BARAKA ZINAPATIKANA HEMANI MWA BWANA. Zaburi 133:1-3 "Tazama, jinsi ilivyo vema, na kupendeza, Ndugu wakae pamoja, kwa umoja. Ni kama mafuta mazuri kichwani, Yashukayo ndevuni, ndevu za Haruni, Yashukayo mpaka upindo wa mavazi yake. Kama umande wa Hermoni ushukao milimani pa Sayuni. Maana ndiko Bwana alikoamuru baraka, Naam, uzima hata milele". Kupitia Efatha ndio mahali tunakopokea Baraka, ila katika kupokea hizo Baraka kuna mpinzani ambae ni ibilisi Shetani anatumia mwanadamu ili kuleta uharibifu na Mungu anatumia mwanadamu vilevile ili kupeleka habari zake, hivyo kwa Efatha anamtumia Mtume na Nabii J. E Mwingira ili kusababisha tufike kwenye Baraka zetu. Katika mazingira yeyote unayopitia iwe ni kazini au kwenye biashara yako zingatia Neno hili ndipo Bwana atatuma waviziao ili kukusaidia. 1wakoritho 16:9 "kwa maana nimefunguliwa mlango mkubwa wa kufaa sana, na wako wengi wanipingao".

MCHUNGAJI DAVID URIO. SOMO:BARAKA ZINAPATIKANA HEMANI MWA BWANA. Yoshua 1:9 "Je! Si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako". Mungu anasema tusiogope maana tumepewa Efatha na jina la Yesu kwa sababu jina la Yesu linafungua, linaponya na kuokoa. Zaburi 24:1-5 "Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana, Dunia na wote wakaao ndani yake. Maana ameiweka misingi yake juu ya bahari, Na juu ya mito ya maji aliithibitisha. Ni nani atakayepanda katika mlima wa Bwana? Ni nani atakayesimama katika patakatifu pake? Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe, Asiyeiinua nafsi yake kwa ubatili, Wala hakuapa kwa hila. Atapokea baraka kwa Bwana, Na haki kwa Mungu wa wokovu wake". Utapokea Baraka kutoka kwa Bwana Mungu wa wokovu wako kupitia jitihada za kukaa kwenye uvuli huu wa Efatha, sikiliza kwa makini maagizo yanayotoka kwa Mtume na Nabii Josephat E. Mwingira na uyatendee kazi maana ndipo zilipo Baraka zako.

MCHUNGAJI DAVID URIO. SOMO:BARAKA ZINAPATIKANA HEMANI MWA BWANA. Zaburi 50:5 "Nikusanyieni wacha Mungu wangu Waliofanya agano nami kwa dhabihu." Sisi tuko hapa kwa sababu mtu mmoja aliweka agano na Mungu . Mithali 16:1 "Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu; Bali jawabu la ulimi hutoka kwa Bwana". ili ung’ae na kupokea Baraka ulizokusudiwa na Mungu ni lazima uwe na maandalizi mazuri. Kumbukumbu 28:1-8 "Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani; na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako. Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani...." Ili uweze kuzipokea hizo baraka kutoka kwa Mungu ni lazima 1. Uwe na sikio la kusikia, je unasikia nini katika Madhabahu ya Bwana kutoka kwa wanao kuongoza? 2. Utii maagizo ya Mungu kutoka kwa viongozi wako haijalishi ni mkubwa au mdogo unachotakiwa ni kutii ili uweze kuziona Baraka za Bwana. Kutoka 23:20 "Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengezea. Jitunzeni mbele yake, mwisikize sauti yake; wala msimtie kasirani; maana, hatawasamehe makosa yenu; kwa kuwa jina langu limo ndani yake." Mbele yako anatangulia malaika wa Bwana ili akulinde ila usimtie kasirani maana hatakusamehe dhambi zako, enenda ukijitiisha chini ya Yesu ili azidi kukulinda na mabaya yote.

Image
Efatha Ministry Mwenge Dar es salaam tunakukaribisha tena katika ibada nzuri leo Jumapili 4/9/2016, popote ulipo Duniani unaweza kufuatilia ibada hizi Kupitia mitandao yetu ya kijamii, na Pia Internet Radio kwenye computer au smartphone yako kupitia link hapo chini. www.mixlr.com/efatha-ministry