MCHUNGAJI DAVID URIO. SOMO:BARAKA ZINAPATIKANA HEMANI MWA BWANA. Zaburi 50:5 "Nikusanyieni wacha Mungu wangu Waliofanya agano nami kwa dhabihu." Sisi tuko hapa kwa sababu mtu mmoja aliweka agano na Mungu . Mithali 16:1 "Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu; Bali jawabu la ulimi hutoka kwa Bwana". ili ung’ae na kupokea Baraka ulizokusudiwa na Mungu ni lazima uwe na maandalizi mazuri. Kumbukumbu 28:1-8 "Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani; na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako. Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani...." Ili uweze kuzipokea hizo baraka kutoka kwa Mungu ni lazima 1. Uwe na sikio la kusikia, je unasikia nini katika Madhabahu ya Bwana kutoka kwa wanao kuongoza? 2. Utii maagizo ya Mungu kutoka kwa viongozi wako haijalishi ni mkubwa au mdogo unachotakiwa ni kutii ili uweze kuziona Baraka za Bwana. Kutoka 23:20 "Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengezea. Jitunzeni mbele yake, mwisikize sauti yake; wala msimtie kasirani; maana, hatawasamehe makosa yenu; kwa kuwa jina langu limo ndani yake." Mbele yako anatangulia malaika wa Bwana ili akulinde ila usimtie kasirani maana hatakusamehe dhambi zako, enenda ukijitiisha chini ya Yesu ili azidi kukulinda na mabaya yote.

Comments