MCHUNGAJI: MELENIA IRENGO SOMO: TABIA Tabia humtambulisha mtu katikati ya watu, tabia yako itakutambulisha kwa watu kuwa wewe ni wa namna gani. Tabia inaweza kumuinua mtu kutoka chini na kumketisha juu. Mfano Mfalme Daudi alikuwa na tabia nzuri tangu akiwa mdogo na Mungu akamuinua kutoka kuchunga kondoo wa Baba yake na kumfanya kuwa Mfalme, tabia nzuri ndiyo inaweza kusababisha ukainuliwa kutoka chini na kuwekwa juu na wafalme. Wagalatia 6:7 “Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.” Unatakiwa ujitathmini mwenyewe kwanza unapanda nini kwa Mungu au kwa watu ili usije ukavuna usicho kitegemea kwa kuwa ukipanda mazuri ndiyo utakayo vuna na pia ukipanda mabaya ndiyo utakayo vuna, panda mema kwa Mungu au watu ili uvune mema. Rumi 8:14 “Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.” ukitaka kutembea na tabia ya Mungu hakikisha unaongozwa na Roho wake maana ukiongozwa na Roho hutafanya yasiyo MPENDEZA MUNGU maana ROHO wa MUNGU ANAKUPA NEEMA jinsi ya kuenenda hapa chini ya jua.


Comments