Posts

Showing posts from March, 2015
Image
UKOMBOZI NA UPONYAJI Ni Kwa Ajili yako; YESU Anakupenda, MUNGU Anakupenda, ROHO MTAKATIFU Anakupenda.

IBADANI JUMAPILI EFATHA MWENGE

Image
SHUHUDA SARA KISINGI: Namshukuru Mungu amenifanyia mambo makuu mawili, nilikuwa sijaokoka nikaja Efatha, nilikuwa nina uvimbe tumboni na nilitakiwa kufanyiwa operation, lakini Askofu wangu akasema hautafanyiwa operation Mungu ni Mwaminifu, nilipofika Kibaha nyumbani, niliendelea kuumwa sana nikapelekwa Amana Hospitali ikashindikana na nilipelekwa Muhimbili lakini baada ya kufika daktari akasema njoo tukupime, baada ya kupimwa akasema kuna jiwe kubwa sana, na akaingiza mkono akalivut a likatoka na akawaita watu waje kunipiga picha kwani mimi ni mtoto wa ajabu nimezaa jiwe, lakini nikamwambia mimi sio mtoto wa ajabu mimi ni mtoto wa Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Baada ya hapo nikaruhusiwa kwenda nyumbani. Pia nilikuwa na kesi ya kusingiziwa, nilipotoka nyumbani kuelekea Polisi nikatamka neno nikasema Mungu mimi hii kesi sio ya kweli naomba unisaidie naingia Polisi naamini nipo na Wewe. Mungu wa Efatha alivyo wa Ajabu, kesi ilienda hadi mahakamani lakini...

IBADANI JUMAPILI TAREHE 22/03/2015

Image
Mchungaji Mary Abel wa Eneo la Utukufu aliyeongoza Ibada ya Neno katika Ibada ya Kwanza..  Efatha Mass wakimuimbia Mungu wetu, hakika wameimba kwa uzuri wa aina yake Mungu azidi kuwapaka mafuta kwa ajili ya utumishi wao. Amen  Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira naye yupo katika Ibada hii ya kwanza ni Baraka ya pekee kuwa na Baba yetu. Amen  Pichani: Mchungaji Thadeo Msuya akihubiri kwenye Ibada ya pili, Efatha Mwenge Dar es salaam.  Watumishi wa Mungu kwa utulivu wakifuatilia Ibada ya Neno iliyoongozwa na Mchungaji Msuya.   USHUHUDA Hery Jackson, namshukuru Mungu kwa kunipa kibali fanya kazi yake Precious Center Kibaha, baada ya kufanya kazi kwa uaminifu, Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira alinikabidhi kwa mtu mmoja akamwambia nenda na huyu kijana ukamfundishe kazi mpaka kitu kitokee, kweli baada ya hapo niliendelea na huyo mtu niliepewa akawa ananifundisha kazi ya uhandisi wa majengo na barabara na kweli kimetokea kitu kam...

WAMAMA AMBAO MMEBARIKIWA HII YA KWENU KUTOKA KWA MAMA YETU.

Image
Wa mama ambao mmebarikiwa, mna maduka Kariakoo, mna Maduka Mwanza, Mna maduka sehemu mbalimbali, mnaenda Dubai, mnaenda China, mmeanza kukosa Uaminifu, hebu ACHENI, hiyo ni dhambi. Hiyo Baraka isikufanye usimuheshimu Mumeo, usimfanye Mumeo housegirl, kama ulikuwa unamuwekea Mumeo Maji endelea kumuwekea, Hela siyo Mume wako, Hiyo ni Maua, najua kuwa MUNGU aliyekupa hizo hela Anakuangalia; Kubali KUBADILIKA, Kubali KUJIREKEBISHA, Acha hiyo Dhambi.

WENYE SAFARI YA MBINGUNI HII INAWAHUSU

Image
Ni lazima Waji Examine, Je pale Nyumbani wanajua Umeokoka? Mkeo anajua Umeokoka? Mumeo anajua Umeokoka? Watoto, Jirani, Wafanyakazi wenzio, Chuoni, Shuleni Wanajua Wewe Umeokoka? Matunda yako ndiyo YATAKAYOSEMA kuwa Wewe Umeokoka, Je hiyo ndivyo ilivyo? Matunda yako yanaonyesha Wewe Umeokoka? Mumeo, Mkeo, Watoto, Jirani na Wote Wanakiri kuwa Wewe Umeokoka? Au unamdhalilisha KRISTO? Jichunguze.

IBADANI TAREHE 16/03/2015 EFATHA MWENGE

Image
SHUHUDA Naitwa Anastazia mmasa namshukuru Mungu kwa yale aliyonitendea nikiwa nina hii mimba ya mtoto huyu nilikuwa nikijisaindia haja ndogo na utumbo mrefu ulikuwaa unatoka nikawa na maumivu makali sana na nilpoenda hospitali mnazi mmoja daktari aliniambia niende muhimbili na lipofika nikakuta kuna foleni sana niliamua kurudi mnazi mmoja wakaniambia nikanunue dawa na nilipoanza kutumia zile dawa nikawa napata maumivu sana na zilikuwa zimebakia dawa za siku tatu nikamwamb ia yesu naomba unihurumie mimi mtumishi wako . Siku za kujifungua zilipofika mama Chitete akaniambia unamwamini Mungu wa Efatha kuwa anaweza ? nikamwambia Amen na muda wa kujifingua ulipofika niliingia leba ya Efatha na mpaka jioni nikawa sijajifungua nikapelekwa mhimbili baada ya muda mfupi nilijifungua salama nikiwa pale hospitali dada mmoja alikuwa anatakiwa afanyiwe upasuaji lakinialiponiona nimejifungua kwa muda mfupi baada ya kufika hospitalini akasema mimi nataka nijifungu k...

IBADANI TAREHE 8/3/2015

Image
Picha mbalimbali Ibada ya kwanza Efatha ministry Mwenge Dar es salaam.

EFATHA MATUKIO NA HABARI MIKOANI NA NJE YA NCHI: Leo tuko Mkoa wa Efatha Ministry- Zanzibar.

Image
Pichani: Viongozi wa Mkoa Efatha Ministry- Zanzibar wakiongozwa na Mch. Kiongozi, wakiwa katika Ukaguzi wa Kupata eneo la Kupanua Kituo kimojawapo cha Mkoa huko Zanzibar.  Pichani: Mchungaji Kiongozi wa Mkoa wa Efatha Ministry -Zanzibar, Mch. Henry akiwa katika Mojawapo ya Safari za Kiutumishi kutembelea Vituo huko Mkoani Zanzibar.  Pichani: Watumishi (Wachungaji) wa Mkoa Efatha Ministry -Zanzibar wakiwa katika Safari ya kwenda eneo la Kituo mojawapo la Efatha Ministry huko Zanzibar (Mbuji) ambapo pia kuna Prayer Mountain ya Mkoa Efatha Ministry- Zanzibar.  Pichani: Wana wa MUNGU wa Efatha Ministry Mkoa wa Zanzibar, wakiwa katika mojawapo za Kazi za Kiroho huko Zanzibar. PIchani: Ibada mojawapo za Uponyaji na Ukombozi huko Zanzibar. (Wewe uliyepo Unguja au Pemba, na ungependa kujumuika kwa pamoja na Wana Wa MUNGU wenzio huko Unguja au Pemba, au unahitaji Msaada wa Kiroho ukiwa huko Pemba au Unguja, basi unaweza kupiga simu hii: 065233834...

EFATHA MATUKIO NA HABARI

Image
Pichani: Mh. Nape akiingia ukumbini Kibaha Precious Centre kuzungumza na Wachungaji wa Efatha.

KUTOKA IBADANI 1/3/2015

Image
MTUMISHI SUZY MSOFE SOMO:WANA WA MUNGU WANATAKIWA WAWAJE Mathayo 5:8 " Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu. " SIFA ZA WANA WA MUNGU 1. Matendo yako yataonekana kwa maana kila utakalolifanya wataliona ni jema. 2. Maneno yako yatakuwa matamu na yakumpa Mungu utukufu. 3. Moyo wako ukiwa safi unakuwa na tabia njema na kuwapendeza hata wanadamu. 4. Wanamtafuta Mungu kwa bidii na wanaongozwa na Mungu na wanakuwa na muda kwa ajili ya Mungu 5. Wanakuwa na njaa na kiu ya neno la Mungu. 6. Wanatamani wengine waingie kwa Yesu ili waone uzuri wa Mungu. 7. Wana wa Mungu wakiudhiwa hawakasiriki, kwa sababu wao wanamtanzama Mungu anasema nini. Pichani: Efatha mass choir wakimwimbia na kumtukuza Mungu wetu mkuu katika Ibada ya kwanza. Mungu wetu anatamani tumuabudu katika Roho na kweli.   Eneo maalum la maombi kwa waliofungwa na vifungo mbalimbali vya kipepo, wakiombewa na kufunguliwa, kwa Jina la Yesu.  MAMA ELIYAKUNDA MWINGIRA Akisalimia kanisa...