IBADANI TAREHE 16/03/2015 EFATHA MWENGE

SHUHUDA

Naitwa Anastazia mmasa namshukuru Mungu kwa yale aliyonitendea nikiwa nina hii mimba ya mtoto huyu nilikuwa nikijisaindia haja ndogo na utumbo mrefu ulikuwaa unatoka nikawa na maumivu makali sana na nilpoenda hospitali mnazi mmoja daktari aliniambia niende muhimbili na lipofika nikakuta kuna foleni sana niliamua kurudi mnazi mmoja wakaniambia nikanunue dawa na nilipoanza kutumia zile dawa nikawa napata maumivu sana na zilikuwa zimebakia dawa za siku tatu nikamwambia yesu naomba unihurumie mimi mtumishi wako . Siku za kujifungua zilipofika mama Chitete akaniambia unamwamini Mungu wa Efatha kuwa anaweza ? nikamwambia Amen na muda wa kujifingua ulipofika niliingia leba ya Efatha na mpaka jioni nikawa sijajifungua nikapelekwa mhimbili baada ya muda mfupi nilijifungua salama nikiwa pale hospitali dada mmoja alikuwa anatakiwa afanyiwe upasuaji lakinialiponiona nimejifungua kwa muda mfupi baada ya kufika hospitalini akasema mimi nataka nijifungu kama huyu dada na kweli ikawa kama alivyosema

Namshukuru Mungu ameniokoa na ajali.
Adam Adam, Namshukuru Mungu nilikuwa naendesha gari aina ya noah nilikuwa naenda Mbeya, nilipofika Iringa lile eneo ambalo gari ya Manjinjah na lori lilipata ajali mimi niliingia kwenye lile shimo lililowaua wenzangu na baada ya hapo gari yangu matairi ya nyuma yalipasuka yote gari likapinduka mara nne lakini sikupata majeraha ya aina yeyote na nilitoka mzima nikiwa na akili zangu zote na kuanza kuwasaidia wenzangu waliokuwa wameumia. Tulikuwa saba kwenye gari mmoja alifariki na wengine walikuwa wamevunjika miguu, viuno na viungo mbalimbali.Neno la madhabahuni linatulinda kwasababu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira alisema hatutakufa kwa ajali, kweli nimeamini Mungu anatembea na wale wampendao. Wana Efatha hatutakufa kwa ajali sawasawa na Neno la Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat E Mwingira.

Shuuda za watumishi wa Mungu waliotumwa Tabora.
Mama mmoja alikuwa kichaa akasema yeye anatokea Msumbiji na anaabudu Sabato hawezi kuoka, wakati tunamuongoza sala ya toba akawa anasinzia, alikuwa na irizi kiunoni imefungwa akasema msiifungue, baada ya maombi kukolea akaifungua ile irizi yeye mwenyewe, baada ya kuombewa kumbe ile nyumba wanashiriki mambo ya kichawi na huyu ni mtu wa Uganda akatoa pembe akatupa nje ile irizi na pembe za uchawi na baadaye akaombewa, na tukaichukua ile irizi na vitu vya uchawi tukavichoma moto, ameokoka na anasoma madarasa Efatha.
Kijana mwingine alisema hawezi kuokoka ana dini yake, baada ya kuongozwa sala ya toba akaanza kusema ana mila na desturi zao, baada ya kuombewa akaanza kusema alikuwa anaumwa, kuna siku alikuwa anakunywa maji inzi aliingia kwenye koo aka kaa hapo mpaka sasa anamiaka 7 bila kutoka hapo kwenye koo, akawa anashindwa kula vizuri na kunywa maji.Pia mke wake hazai wala hawana mtoto,baada ya kuombewa na watumishi wa Mungu wa Efatha inzi akatoka katika koo lake, amesimama katika wokovu na anasoma madarasa na mke wake,hivi sasa mke wake ni mjamzito.Anamshukuru Mungu wa Efatha kwa matendo makuu aliyo mtendea.
Dada mmoja anaitwa Asha alikuwa mchawi na baada ya watumishi wa Mungu kumuombea walimchukua na kuishi nae,lakini akajaribu kuwawangia watumishi wa Mungu usiku waka mkamata, alipoendelea kuombewa alikataa kuacha uchawi, Watumishi wa Mungu walimrudisha kwao na kumuonya kama hataki kuacha uchawi atakufa, baada ya siku chache akafa kutokana na nguvu ya Mungu. Kama ilivyo andikwa usimwache mchawi aishi.
 Pichani: Mch. Thadeo Msuya aliyesimama katika Ibada ya Neno Ibada ya pili.
 Katika Picha: Ibada za watoto ambapo watoto hufundishwa kulingana na umri wao, wana waalimu maalum walioandaliwa ili kuwalea na kuwafundisha watoto. Ni vizuri kuwalea watoto katika Mungu ili wawe na msingi mzuri wa Imani. Unapokuja Ibadani na mwanao usihofu wakati wewe ukiwa kanisani, mwanao atakuwa kwenye ibada zao maalum. Karibu sana na Mungu akubariki


 Pichani: Kanisa likiwa katika maombi Ibadani. Live Ibada ya kwanza
 Pichani: Wana wa Mungu wakiwa katika Ibada ya maombi Ibada ya kwanza Efatha mwenge Dar es salaam Tazania

Comments