KUTOKA IBADANI 1/3/2015

MTUMISHI SUZY MSOFE
SOMO:WANA WA MUNGU WANATAKIWA WAWAJE
Mathayo 5:8 " Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu.
"
SIFA ZA WANA WA MUNGU
1. Matendo yako yataonekana kwa maana kila utakalolifanya wataliona ni jema.
2. Maneno yako yatakuwa matamu na yakumpa Mungu utukufu.
3. Moyo wako ukiwa safi unakuwa na tabia njema na kuwapendeza hata wanadamu.
4. Wanamtafuta Mungu kwa bidii na wanaongozwa na Mungu na wanakuwa na muda kwa ajili ya Mungu
5. Wanakuwa na njaa na kiu ya neno la Mungu.
6. Wanatamani wengine waingie kwa Yesu ili waone uzuri wa Mungu.
7. Wana wa Mungu wakiudhiwa hawakasiriki, kwa sababu wao wanamtanzama Mungu anasema nini.

Pichani: Efatha mass choir wakimwimbia na kumtukuza Mungu wetu mkuu katika Ibada ya kwanza. Mungu wetu anatamani tumuabudu katika Roho na kweli.

 
Eneo maalum la maombi kwa waliofungwa na vifungo mbalimbali vya kipepo, wakiombewa na kufunguliwa, kwa Jina la Yesu.

 MAMA ELIYAKUNDA MWINGIRA Akisalimia kanisa katika Ibada ya kwanza.

 Pichani: Mojawapo ya Ibada ya watoto (sunday school) hapa Efatha Mwenge Dar es salaam. Watoto huwa na Ibada zao maalum na waalimu wao maalum kuwafundisha, kuwalea na kuwaombea watoto. Ni ibada nzuri sana kwa watoto,walikuwa na mitihani ya kile wanachofundishwa. Mlee mtoto katika njia inayofaa naye hataicha katika maisha yake yote.

Comments