IBADANI JUMAPILI EFATHA MWENGE

SHUHUDA

SARA KISINGI: Namshukuru Mungu amenifanyia mambo makuu mawili, nilikuwa sijaokoka nikaja Efatha, nilikuwa nina uvimbe tumboni na nilitakiwa kufanyiwa operation, lakini Askofu wangu akasema hautafanyiwa operation Mungu ni Mwaminifu, nilipofika Kibaha nyumbani, niliendelea kuumwa sana nikapelekwa Amana Hospitali ikashindikana na nilipelekwa Muhimbili lakini baada ya kufika daktari akasema njoo tukupime, baada ya kupimwa akasema kuna jiwe kubwa sana, na akaingiza mkono akalivuta likatoka na akawaita watu waje kunipiga picha kwani mimi ni mtoto wa ajabu nimezaa jiwe, lakini nikamwambia mimi sio mtoto wa ajabu mimi ni mtoto wa Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Baada ya hapo nikaruhusiwa kwenda nyumbani.
Pia nilikuwa na kesi ya kusingiziwa, nilipotoka nyumbani kuelekea Polisi nikatamka neno nikasema Mungu mimi hii kesi sio ya kweli naomba unisaidie naingia Polisi naamini nipo na Wewe.
Mungu wa Efatha alivyo wa Ajabu, kesi ilienda hadi mahakamani lakini mawakili walianza kugombana wao kwa wao, nikaambiwa niondoke kwani kulionekana hakuna kesi walikuwa wamenisingizia kesi ya uongo. Nikaruhusiwa nikaondoka. Namshukuru Mungu wa Baba yangu Mtume na Nabii Josephat E Mwingira kwa matendo makuu Aliyonitendea.

Anastella Mchomvu: Ninamshukuru sana Mungu wa Efatha kwa ajili ya matendo makuu aliyonitendea. Wakati nakwenda Kusanyiko Kuu Kibaha Mwaka jana nilikuwa natafuta mashamba na nilikuwa natamani mashamba makubwa na nilipofika Kusanyiko Mtumishi wa Kenya akawa anafundisha somo la "Mimi ni mtu Mkubwa sana", Usiku ule nilifanya maombi na nikajibiwa usiku ule ule, nikapigiwa simu kuwa kuna mashamba Morogoro, na baada ya kutoka Kusanyiko mimi na Mume wangu tulienda Turiani Morogoro tukapewa mashamba makubwa kwa bei ya ajabu, na nilipata hekari 200 kwa ajili ya kulima, pia tumenunua hekari 10 kwa ajiri ya Efatha, na nimekuja na hati ya mauziano ya hekari 10 kwa ajili ya Efatha.
Pia Bagamoyo nimepata hekari 100, pia napenda kumshukuru Mungu kwa kunipatia Nyumba kwani jana tarehe 28/03/2015 nimefanya ibada ya kuweka wakfu nyumba yetu, Mungu wa Efatha amenifanyia maajabu.
Pia tulikuwa tumetoka kuwaona wazazi, tulipofika Tabata tulipata ajali iliyosababisha magari 4 kugongana lakini kwenye gari yetu hatukuumia, kwani nilimwambia Mungu hili gari nililiweka wakfu kwa ajili ya kazi yako.
Pia napenda kumshukuru Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira na Watumishi wote walio kuwa wananiombea.
 Hongereni wote mliompokea Bwana Yesu leo, kwa nguvu yake awawezeshe wote kuishi maisha ya ushindi INAWEZEKANA kuishi maisha Matakatifu hapa Duniani. Kuanzia leo kushindwa siyo sehemu ya maisha yenu Ibilisi ameshindwa kabisa.

Comments