IBADA KUU TAREHE 25/01/2015 EFATHA MWENGE.
Mchungaji kiongozi Kanisa la Efatha Mwenge Dar es salaam akifundisha katika Ibada ya kwanza. USHUHUDA Naitwa Vicent Sungura. Mimi napenda kumshukuru Mungu kwa yale aliyonitendea, Baba alisema tukagombee nafasi mbalimbali kwenye maeneo tunayoishi nikagombea ujumbe wa serikali ya mtaa, mtaa wa mabibo, katika kura za maoni nilishinda kwa kishindo mpaka kusimama kuwa mjumbe. Pia napenda kumshukuru Mungu kuwa nilikwenda nyasa kwetu kutangaza nia ya kugombea udiwani nilipofika songea mjini nikapigiwa simu kwamba kuna kazi ya ICT Kigoma, baadaye nilipigiwa simu nikaambiwa kuna kazi nyingine Mwanza. Wakati naingia Efatha nilimuamini mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira nikaamua kushika maneno anayotufundisha nikaazimia mambo matatu, nilisema nitakuwa mwimbaji nimuimbie Mungu, imekuwa. Pia nilisema kwa namna yeyote nitasoma Mungu ni mwema nilipata mfadhili Naibu waziri wa miundo mbinu nimesoma mpaka chuo kikuu, nikasema nitafanya kazi nitakayoichagua yenye ...