IBADA KUU Tarehe 18/01/2015 EFATHA MWENGE.

TABIA
....Tabia zipo za aina mbili ya kwanza ni tabia nzuri ambayo inatokana na Mungu na tabia mbaya asili yake ni shetani.
....Kutoka kwenye tabia ya dhambi siyo rahisi ndiyo maana tunamwitaji Yesu
...Unapookoka umasamehewa dhambi na unatengwa na uovu
...Unaporudi katika maisha ya dhambi unajitenga na Mungu
....Wokovu unaupokea moyoni na unadhihirishwa kwa matendo yako.
....Katika kutembea na Mungu tabia yako ni lazima ifanane na tabia ya Mungu.

 Mchungaji: Mwakisole .

USHUHUDA
Naitwa Felista Benjamini, napenda kumshukuru Mungu kwa kunipa kibali cha kujifungua bila upasaji, ilikua si rahisi lakini kwa neema yake Mungu wakati wakujifungua ulipofika niliambiwa njia haionekani japokuwa mtoto alikuwa kageuka kwa ajili ya kutoka haikuwezekana kwani njia ilikuwa haionekani. Ikabidi nipelekwe Hospitali ya Muhimbili, nilipofika daktari wa kunifanyia upasuaji hakuwepo, alikuwa kufanya upasuaji kwa mtu mwingine. Mimi sikuacha kuomba nikimsihi Mungu nikamwambia Mungu kama Mama Maria(Yesu) alijifungua kwa upasuaji, basi na mimi nitajifungua kwa upasuaji. Kama Maria(Yesu) alijifungua kwa kuongezewa njia basi na mimi nitaongezewa, baada ya kusema na Mungu, ilikuwa kama muujiza kwangu nilimwambia Mungu kwamba mtoto anatakiwa atokee sehemu aliyoingilia.
Basi niliendelea kumsihi Mungu kwa hilo baadaye nilipofikia zamu yangu kuingizwa chumba cha upasuaji nilimwambia Mungu nakuomba unipe nguvu ya kusukuma kwani Roho wa Bwana yu juu yangu! basi nilijikuta Napata nguvu ya ajabu nikasukuma na mtoto akatoka walishangaa kuona vile, lakini najua kwa kuwa huu ni mwaka wangu wa Mtembeo wa Mungu basi Mungu hakuniacha peke yangu Amina.

Pichani: Mama Eliakunda Mwingira ibadani tarehe 18.1.2015
Pichani: Watumishi wa Mungu wakiwa ibadani wakifuatilia kwa makini maagizo kutoka madhabahuni.. Jumapili tarehe 18.1.2015
 Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira akisikiliza Neno katika Ibada ya Pili iliyoongozwa na Mchungaji wa Eneo la Sayuni Mchungaji Aimana Dominick

Comments