Yohana 5:17-18 "Akawajibu, Baba yangu anatenda kazi hata sasa, nami ninatenda kazi. Basi kwa sababu hiyo Wayahudi walizidi kutaka kumwua, kwa kuwa hakuivunja sabato tu, bali pamoja na hayo alimwita Mungu Baba yake, akijifanya sawa na Mungu. Basi Yesu akajibu, akawaambia, Amin, amin, nawaambia," Hoja kubwa ya wayahudi kumkarikia Yesu ni juu ya SABATO, na hadi leo hii kuna ubishani mkubwa juu ya siku ya sabato. Sabato maana yake ni puumziko, siyo siku, uwe na siku ya kupumzika uiheshimu. Mungu alifanya kazi siku sita ya saba akapumzika hapa haoneshi siku bali alifanya kazi siku sita Mungu akaona kazi ni njema, akapumzika. wewe unapumzika vipi kama hujamaliza kazi? wanadamu wengi leo wanapumzika bila kumaliza kazi Mwanzo 2:1-2 "Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote. Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. " Mungu alipoona amekamilisha kazi alifurahia akapumzik...