SOMO: KAZI ZA YESU.
Yohana 5:17-18 "Akawajibu, Baba yangu anatenda kazi hata sasa, nami ninatenda kazi.
Basi kwa sababu hiyo Wayahudi walizidi kutaka kumwua, kwa kuwa hakuivunja sabato tu, bali pamoja na hayo alimwita Mungu Baba yake, akijifanya sawa na Mungu. Basi Yesu akajibu, akawaambia, Amin, amin, nawaambia,"
Hoja kubwa ya wayahudi kumkarikia Yesu ni juu ya SABATO, na hadi leo hii kuna ubishani mkubwa juu ya siku ya sabato.
Sabato maana yake ni puumziko, siyo siku, uwe na siku ya kupumzika uiheshimu. Mungu alifanya kazi siku sita ya saba akapumzika hapa haoneshi siku bali alifanya kazi siku sita Mungu akaona kazi ni njema, akapumzika. wewe unapumzika vipi kama hujamaliza kazi? wanadamu wengi leo wanapumzika bila kumaliza kazi
Mwanzo 2:1-2 "Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote.
Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. "
Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. "
Mungu alipoona amekamilisha kazi alifurahia akapumzika kwa maana nyingine isingekamilika asinge pumzika, usipumzike kwa sababu ya siku bali kwa sababu umekamilisha.
Mathayo:12 :1-8 “Wakati ule Yesu alipita katika mashamba siku ya sabato; wanafunzi wake wakaona njaa, wakaanza kuvunja masuke, wakala. Na Mafarisayo walipoona, walimwambia, Tazama! Wanafunzi wako wanafanya neno ambalo si halali kulifanya siku ya sabato. Kwa maana Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato.
Chombo sio kikubwa kama mtumiaji wa chombo, siku siyo muhimu kama wewe. Anamaanisha nini anaposema mwana wa adamu anaondoka katika uungu anahusisha ubinadamu wetu. Sabato imewekwa kwa ajili ya mwanadamu, mapumziko hayahusu siku tu bali mapumziko ya kweli kutoka katika vifungo mbalimbali
Mathayo 11;28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.”
Mimi ndiye Bwana wa sabato “mimi bwana wa mapumziko” yeye ndiye atupaye pumziko, hazungumzii siku. Siku, miaka na nyakati zipo kwetu ili ujue yakupasayo kutenda kwamba ni wakati wa kusoma, kuoa.Siku haipumzishi bali mtu anapumzika na anayempumzisha mtu ni Bwana wa napumziko Yesu pekee, hakuna msaada katika siku.

Yohana 5:39 "Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia."
Wewe nabaki kuchunguza chunguza maandiko katika biblia ukizani huko kuna mzima, chunguza sana Yesu asomewi Yesu anaaminiwa, kuna watu wanaisomea biblia miaka mingi hadi vipara lakini hawana Roho Mtakatifu na hawawezi kuombea wagonjwa.

Usifungwe na siku maana kwa Mungu wetu kila siku ni siku ya Mungu, wewe ndiye unayechagua lini nipumzike. Kumbuka pumziko la kweli lipo kwa Bwana Yesu. Yesu alipomaliza kazi aliacha maagizo kwa watumishi aliowaweka ila wafanye na wawaelekeze watu wafanye kile Yesu amekusudia wafanye ikiwa ni pamoja na kuwapumzisha wenye mateso na vifungo mbalimbali ikiwa ni pamoja na magonjwa ma mateso mbalimbali.
Leo hii tunashuhudia watu wakipata mapumziko katika ndoa zao, afya zao, uchumi wao, Walio katika kristo ni marufuku kupita katika mateso, maana unaye apumzishaye. Hakuna maisha ya raha na amani kama ya WOKOVU.
Comments
Post a Comment