Neno La leo na Mchungaji Aimana.
NENO LA
JUMAPILI NA MTUMISHI WA MUNGU AIMANA DOMINIC
Mwanzo 4:7a. kama ukitenda vyema hutapata kibari? angalia
ushuhuda wa huyu dada kwamba aliona hana haja ya kusema atafauru lakini alijifuta mwenyewe. mangapi
yametamkwa kwenye madhabahu ya Mungu lakini kwako hayajatimia kwa sababu
tunashindwa kujitakia mema? Kama yale yaliyo tamkwa kwangu na tungeyatakia mema
yale tungekua mbali. Nipo hapa kukukumbusha achana na zile nyaraka ambazo
zimeandikwa na wanadamu angalia nyaraka za kwenye Bibilia.
Tukiamua
kubadilika tukabeba nyaraka za madhabahuni tutakua na ushuhuda kabla mwaka
haujaisha. Nenda katafute Yule mtu mwenye dhambi anaye jiuza anaye piga miziki
disko mlete kwa Yesu wapo tayari wanatusubiri tuwaendee.
Umepakwa
mafuta ya Roho Mtakatifu je unayatendea mema yale mafuta? kwenye kamati haupo
ivi hayo mafuta yako unayatendea mema. Sababisha mchungaji wako wa kituo
afurahi angalia unaweza kufanya nini hemani mwa bwana fanya usababishe Yesu
afurahi.
Comments
Post a Comment