Wana wa MUNGU walioamua kuja kwa YESU
Nendeni duniani kote mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi wangu... Ni agizo la BWANA wetu YESU KRISTO kuwaleta watu kwake, kuwaleta watu kwenye NURU, kuwaleta kwenye kuwekwa HURU, lazima tutafute kilichopotea, Tutafute Kondoo, wengi bado wanateseka katika mamlaka ya nguvu za giza, wakati YESU Alikufa kwa ajili yetu, hebu timiza agizo hili mlete mtu kwa YESU ili naye aondokane na mateso anayopata, huo ndio UPENDO. Pichani: Wana wa MUNGU walioamua kuja kwa YESU, walioamua kuyakabidhi maisha yao kwa BWANA wetu YESU KRISTO, na tunamshukuru MUNGU wetu MUNGU MKUU kwa kutupa Kibali na Neema cha kuwaleta watu kwa YESU KRISTO BWANA wetu kila Ibada, kila Jumapili Efatha Ministry Mwenge, Dar es Salaam, Tanzania.