IBADA YA JUMAPILI 18/8/2014

PICHA MBALIMBALI Ibada ya Leo

 Zaituni Mteiya – Shaloom – sikuwahi kuonana na Baba yangu tangu 2005 pia sijaonana na mama yangu aliyeolewa Ulaya. Alipoenda ulaya hakutaka kabisa kuwasiliana na sis watoto wake aliwashirikisha watumishi kuhusu jambo hilo, siku moja Mtume na Nabii alitamka kwamba mwezi huu Mungu ataenda kuwashangaza watu. Mwaka mmoja ulio pita mama alikuwa anawasiliana na mume wangu lakini, alikuwa hatujali wanawe kwa lolote, alikuwa akiwajali na kuwanunulia ndugu zake nyumba na vitu vingine. Mungu alinishangaza baada ya mama yangu kupiga simu na kutaka kuongea na nami aliniomba nimwandalie hotel wakati sio kitu cha kawaida alipokuja mama alinipa pesa nyingi, gari aina ya URO, anamshukuru Mungu sana.
Mariamu Mdosa – Shaloom : Mwanafunzi chuo cha muhimbili ninasomea mionzi namshukuru Mungu kwa hilo moja, katika chuo ninachosoma tulitakiwa kuandaa project na mimi nilikuwa sina ujuzi kuhusu kuandaa project. Lakini mwezi huu nilikuwa nimekaa na kufikiri nikamuuliza Bwana Yesu, nitaongea nini siku ya kwanza? nilitiwa ufahamu nikaanza kuandaa kazi kwa muda wa siku tatu nikapata presentation. sijawahi kusimama na kuongea, na nikafanya presentation vizuri nikaweza kushinda na kuwa wa kwanza presentation hiyo ilifanyika katika ukumbi wa karimjee. Ninamshukuru Mungu kwa hilo. Mtu wa Mungu Hakuna kinachomshinda Yesu. Popote ulipo, chochote unachofanya litumie Jina la Yesu kwa imani itakuwa. Mungu akuwezeshe. Live Ibada ya Pili Efatha Mwenge
 

Comments

Popular posts from this blog

Mithali 8:17-21 "Nawapenda wale wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidii wataniona. Utajiri na heshima ziko kwangu, Naam, utajiri udumuo, na haki pia. Matunda yangu hupita dhahabu, naam, dhahabu safi, na faida yangu hupita fedha iliyo teule. Natembea katika njia ya haki, katikati ya mapito ya hukumu. Niwarithishe mali wale wanipendao, tena nipate kuzijaza hazina zao." Proverbs 8: 17-21 "I love them that love me; and those that seek me early shall find me. Riches and honour are with me; yea, durable riches and righteousness. My fruit is better than gold, yea, than fine gold; and my revenue than choice silver. I lead in the way of righteousness, in the midst of the paths of judgment: That I may cause those that love me to inherit substance; and I will fill their treasures."