Posts

Image
SOMO: "ACHA WOGA NA MFADHAIKO." Kuna watu ambao wakitishwa na maneno, shinikizo la damu linaongezeka na wanapata magonjwa kwa haraka. Watu wengine hawana uwezo wa kustahimili misukosuko ya maisha mfano Kustaafu, kuachishwa kazi, kudhulumiwa, na kadhalika. Mara nyingi watu wenye mfadhaiko namna hii wakiacha woga watakuwa na MAFANIKIO. Mtu anapoacha woga na Kumtumikia Mungu inamfanya Mungu akae naye wakati wote. Mungu hana woga na amesisitiza mahali pengi katika Biblia juu ya k uwa JASIRI na kumtegemea YEYE. Mtume Paulo anakazia hoja hii alipomwandikia Timoteo; IITimoteo 1:6-7 "Kwa sababu hiyo nakukumbusha, uichochee karama ya Mungu, iliyo ndani yako kwa kuwekewa mikono yangu. Maana Mungu hakutupa Roho ya woga, bali ya NGUVU na ya UPENDO na ya moyo WA KIASI". Kila mtu ambaye amewahi kuwekewa mikono na Mpakwa Mafuta wa BWANA, amejiwa na NGUVU ya Roho wa Mungu ndani yake, hivyo achochee hiyo karama iliyoko ndani yake. Aache woga, asonge mbele na Mungu atakuwa na...
Image
SOMO: “KUONGEZA VIWANGO KUPITIA UUMBAJI WA UTAJIRI.” Huwezi kuheshimika katika taifa lolote isipokuwa pale unapotangaza UTAJIRI wako. Umaskini sio wa UFALME wa Mungu, na katika UFALME wa Mungu, umaskini sio mwanachama; kwa sababu umaskini hauna Utukufu. (Mungu wetu ni MUNGU WA UTUKUFU). Wamisionari walipokuja Afrika, walitufundisha tu kuhusiana na toba lakini hawakutufundisa kuhusu “UUMBAJI wa UTAJIRI” katika Wokovu. Wamisionari waliwafanya Waafrika wasiwaze kuusu USTAWI lakin i walitufanya tuwaze kuhusu kwenda Mbinguni tu. Kabla hujaenda Mbinguni, Mungu anataka wewe UFANIKIWE hapa duniani. Ingawa Yesu alikuja kutafuta wenye dhambi na waliopotea, lakini hakukutana na kukaa na kila mtu isipokuwa Zakayo alipata Kibali kwa sababu ya mambo kadhaa; Zakayo alionekana kwa urahisi na Yesu kwa sababu ya mambo yafuatayo; 1. Jina lake lilikuwa Mashuhuri (alikuwa na cheo). 2. Alikuwa ni mwana taaluma, msomi na mchapakazi. 3. Alikuwa tajiri. 4. Tamanio la Moyo wake ilikuwa ni kumuona Yesu. ...
Image
TOPIC: "RAISING STANDARDS THROUGH WEALTH CREATION" You cannot be respected in any nation unless you declare your Wealth. Poverty is not of the Kingdom, and in the Kingdom of God poverty is not a member since poverty has no Glory. (Our God is a GOD of Glory). When the missionaries came to Africa they only taught us to repent but they did not talk about WEALTH in salvation. The missionaries made the Africans not to think about Prosperity but they just made us to think about liv ing the earth. Before you go to heaven, God wants you to be SUCCESSFUL here on earth. Despite that Jesus came to seek the sinners and those who were lost, He did not meet and sit with every person but Zacchaeus got favor because of the reasons below; Zacchaeus was quickly spotted out by Jesus because of these reasons; 1. His name was noble. 2. He was a professional, educated and he was working. 3. He was very rich. 4. The desire of his heart was to see Jesus. Everyone here on earth was created ...
Image
Naibariki Jumatano yangu, Jumatano yangu IMEBARIKIWA na BWANA, Jumatano yangu Imevikwa TAJI YA BARAKA na WEMA WA MUNGU Aliye BABA Yangu wa Mbinguni, NITAFURAHI na KUSHANGILIA maana YEYE Ananipenda na Kunijali, Jumatano yangu IMEBARIKIWA, Asante YESU Nakupenda BWANA.
Image
SOMO: “NGUVU YA MUNGU” NGUVU ni nini? NGUVU maana yake ni UHAI. NGUVU ya Mungu ni ya muhimu sana kwa MWAMINI. Kuna Nguvu ya kutembea, kuona, kuoa na kuolewa, nguvu ya kupata watoto n.k… Mfano: kuna Nguvu inayowezesha macho yapate kuona, mara hiyo Nguvu inapoondoka mtu hutafuta miwani ili imsaidie kuona. Ili uweze kutembea kwa uimara katika WOKOVU, lazima uwe na NGUVU ya Mungu. Matendo 1:8 "Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi." Unapoipokea NGUVU ya Mungu ndipo unakuwa na uwezo wa KUSHUHUDIA na kufanyika SHAHIDI. Roho Mtakatifu ndiye ANAYEKUWEZESHA kufanyika shahidi. Bila Nguvu ya Mungu, unakuwa kama mtu asiyekuwa na miguu, lakini ukiwa na Nguvu ya Roho Mtakatifu; hakuna cha kukuzuia. Watu lazima wajue kuwa wewe UMEOKOKA na ni mali ya Kristo. Lakini inawezekana tu kupitia Nguvu hii ya Roho Mtakatifu. - Pasipo NGUVU ya ROHO MTAKA...
Image
Naibariki Jumanne yangu, YESU NI MZURI, YEYE Ni Mwenye REHEMA tele, Mwanangu FURAHI na KUSHANGILIA, HUTASHINDWA bali UTASHINDA, Huu ni MWAKA NGUVU YA MUNGU, NGUVU YA MUNGU Itakujilia KUKUSHINDIA YOOOTE, FURAHI Mwanangu, MUNGU ANAKUPENDA, Lazima UTASHINDA, FURAHI,..... Jumanne yako IMEBARIKIWA.
Image
GOD WANTS US TO RISE UP THROUGH TEACHINGS PASTOR MAGRETH ILOMO (Efatha Mwenge). You cannot rise up if you are not TAUGHT. Therefore you have to accept to be taught. Do not be worried about the things which you are not aware of, since God will teach you and guide you if you are ready to LEARN. Proverbs 4:13 “Take fast hold of instruction; let her not go: keep her; for she is thy life.” Use much of your TIME to LEARN than PRAYING. If at first you had used much of your TIME to pray, now desire to use much of your TIME to LEARN about God through the bible and by reading books written by HIS SERVANTS. Fill your TANK (heart & mind) through LEARNING and READING the WORD of God. It’s a matter of CHOICE, if you want to be GREAT use much of your TIME to LEARN. GOD wants us to RECOGNIZE ourselves, “who we are” here on earth. If you don’t recognize who you are, the devil will torture you. But once you take much of your TIME to LEARN, you will RECOGNIZE who you are and...