SOMO: "ACHA WOGA NA MFADHAIKO."
Kuna watu ambao wakitishwa na maneno, shinikizo la damu linaongezeka na wanapata magonjwa kwa haraka. Watu wengine hawana uwezo wa kustahimili misukosuko ya maisha mfano Kustaafu, kuachishwa kazi, kudhulumiwa, na kadhalika. Mara nyingi watu wenye mfadhaiko namna hii wakiacha woga watakuwa na MAFANIKIO. Mtu anapoacha woga na Kumtumikia Mungu inamfanya Mungu akae naye wakati wote. Mungu hana woga na amesisitiza mahali pengi katika Biblia juu ya kuwa JASIRI na kumtegemea YEYE. Mtume Paulo anakazia hoja hii alipomwandikia Timoteo;
IITimoteo 1:6-7 "Kwa sababu hiyo nakukumbusha, uichochee karama ya Mungu, iliyo ndani yako kwa kuwekewa mikono yangu. Maana Mungu hakutupa Roho ya woga, bali ya NGUVU na ya UPENDO na ya moyo WA KIASI".
Kila mtu ambaye amewahi kuwekewa mikono na Mpakwa Mafuta wa BWANA, amejiwa na NGUVU ya Roho wa Mungu ndani yake, hivyo achochee hiyo karama iliyoko ndani yake. Aache woga, asonge mbele na Mungu atakuwa naye. Kila jambo atakalofanya atauona UWEZA wa Mungu Haleluya!
   : Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira - Efatha Ministry.

Comments