SOMO: “NGUVU YA MUNGU”
NGUVU ni nini? NGUVU maana yake ni UHAI.
NGUVU ya Mungu ni ya muhimu sana kwa MWAMINI. Kuna Nguvu ya kutembea, kuona, kuoa na kuolewa, nguvu ya kupata watoto n.k… Mfano: kuna Nguvu inayowezesha macho yapate kuona, mara hiyo Nguvu inapoondoka mtu hutafuta miwani ili imsaidie kuona.
Ili uweze kutembea kwa uimara katika WOKOVU, lazima uwe na NGUVU ya Mungu.
Matendo 1:8 "Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi."
Unapoipokea NGUVU ya Mungu ndipo unakuwa na uwezo wa KUSHUHUDIA na kufanyika SHAHIDI. Roho Mtakatifu ndiye ANAYEKUWEZESHA kufanyika shahidi. Bila Nguvu ya Mungu, unakuwa kama mtu asiyekuwa na miguu, lakini ukiwa na Nguvu ya Roho Mtakatifu; hakuna cha kukuzuia.
Watu lazima wajue kuwa wewe UMEOKOKA na ni mali ya Kristo. Lakini inawezekana tu kupitia Nguvu hii ya Roho Mtakatifu.
- Pasipo NGUVU ya ROHO MTAKATIFU, huwezi kuishinda DHAMBI. NGUVU ya Mungu ndiyo inakuwezesha kuushinda MWILI na TABIA zake mfano; uzinzi, uasherati, n.k..
UELEWA ndiyo unaokupa NGUVU. Elewa kuwa UNAPENDWA na Mungu; hivyo sogea kwa ujasiri mbele zake pale unapokuwa na uhitaji wa chochote.
Kwa kadri unavyosogea karibu na Mungu, “siku kwa siku” ndivyo unavyo pokea NGUVU ya Mungu, afya njema na uwezo wa kufanya mambo yote.
Wafilipi 4:13 “Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.”
© Mama Eliakunda Mwingira (Efatha Ministry).

Comments