SOMO: “KUONGEZA VIWANGO KUPITIA UUMBAJI WA UTAJIRI.”
Huwezi kuheshimika katika taifa lolote isipokuwa pale unapotangaza UTAJIRI wako.
Umaskini sio wa UFALME wa Mungu, na katika UFALME wa Mungu, umaskini sio mwanachama; kwa sababu umaskini hauna Utukufu. (Mungu wetu ni MUNGU WA UTUKUFU). Wamisionari walipokuja Afrika, walitufundisha tu kuhusiana na toba lakini hawakutufundisa kuhusu “UUMBAJI wa UTAJIRI” katika Wokovu. Wamisionari waliwafanya Waafrika wasiwaze kuusu USTAWI lakini walitufanya tuwaze kuhusu kwenda Mbinguni tu.
Kabla hujaenda Mbinguni, Mungu anataka wewe UFANIKIWE hapa duniani. Ingawa Yesu alikuja kutafuta wenye dhambi na waliopotea, lakini hakukutana na kukaa na kila mtu isipokuwa Zakayo alipata Kibali kwa sababu ya mambo kadhaa; Zakayo alionekana kwa urahisi na Yesu kwa sababu ya mambo yafuatayo;
1. Jina lake lilikuwa Mashuhuri (alikuwa na cheo).
2. Alikuwa ni mwana taaluma, msomi na mchapakazi.
3. Alikuwa tajiri.
4. Tamanio la Moyo wake ilikuwa ni kumuona Yesu.
Kila mmoja hapa duniani aliumbwa ili awe TAJIRI, kwa sababu nasaba zetu zinaendana na zile za MUNGU (Na Mungu ni TAJIRI sana). Ukijiringanisha wewe na watu wengine, unaipoteza njia; kwa sababu Mungu alikuumba wewe katika UTOFAUTI. Sababu pekee kwa nini wewe unajichukulia kuwa maskini ni kwa sababu UNAJIRINGANISHA na wengine; lakini siku utakapoacha kujiringanisha na wengine, ndiyo siku utakapojijua kuwa wewe ni wa Kipekee.
Luka 19:4 “Akatangulia mbio, akapanda juu ya mkuyu apate kumwona, kwa kuwa atakuja kuipitia njia ile.”
Unapoamini unatakiwa KUCHUKUA HATUA. Zakayo alienda mbele ya wale walioshindana nae. Mara zote unapoinena ndoto yako, elewa kuwa wengi watainuka ili kushindana na wewe. Mungu sio dhalimu, hivyo yeyote anayejinyenyekeza mbele zake, atamuona. Zakayo alielewa siri hii, ikampelekea kwenda mbele ya wengine.
MAWAZO yako ndiyo yatakayokutofautisha na wengine. Wengine wakilalamika kuhusiana na umaskini wewe achana nao na usijari bali SONGA MBELE yao na ukawe TAJIRI mbele ya macho yao; ukishafanikiwa watakufuata.
“WEWE SIO MASKINI, BADILISHA TU NAMNA UNAVYOWAZA.”
© ASKOFU CHARLES KARIUKI.

Comments