Posts

Showing posts from August, 2017

SOMO: NEEMA YA BWANA YESU.

Image
ZIARA YA KITUME NA KINABII MKOA WA KIGOMA. SOMO: NEEMA YA BWANA YESU. NEEMA ni ya Bwana YESU, UPENDO ni wa Mungu BABA na USHIRIKA ni wa ROHO MTAKATIFU. NEEMA ni Nini? Neema ni kitu ambacho mtu Anaweza kukipata pasipo kustahili. Tumeokolewa kwa Neema, sisi tulikuwa ni wenye dhambi na wala hatukustahili kuokolewa, lakini kwa Neema ya Bwana YESU tumepata kuokolewa. Kwa nini Neema? Neema ndiyo inayokufungulia ili uweze kufika mahali ambapo utakuwa na SHUKRANI kwa Mungu, bila Neema huwezi kuwa na SHUKRANI. Kwa nini mtu mwenye Neema anakuwa na Shukrani? Ni kwa sababu ametendewa kitu ambacho hakutarajia kukipata. Jambo lolote ambalo unalipata pasipo tarajio na likakupa wewe Ahueni, Nafuu au Faraja hiyo ndiyo inaitwa NEEMA. Neema ni ya muhimu sana kwa mtu yeyote yule Anayetamani kwenda mbele, awe ameokoka au hajaokoka, mtu akishafikiwa na Neema anakuwa na Changamko katika Maisha yake na SHUKRANI kwa Mungu wake, bila NEEMA hakuna Changamko wala Shukrani. ITAMANI NEEMA KATIKA MAISHA ...
Image
ZIARA YA KITUME NA KINABII MKOA WA KIGOMA. SOMO: NEEMA YA BWANA YESU. Kazi ya Neema ni kuondoa HUZUNI na MACHUNGU, usione mtu ana HUZUNI au MACHUNGU ukajua kuwa hana UPENDO, La! Anao lakini kuna kitu kimekosekana kwake ambacho ni NEEMA; akipata NEEMA changamko linatokea katika Maisha yake.    • NEEMA ikikosekana kwako maswali yanakuwa mengi juu yako, Mtu mwenye NEEMA huwa hakataliwi popote pale atakapokwenda.    • Ili uweze Kuchanua unahitaji NEEMA, ukiwa mwanaume ni lazima NEEMA izidi kwako ili uweze kusababisha jambo litokee katika Maisha na Familia yako kiujumla.    • NEEMA ndiyo inayokuhalalisha wewe uweze Kukubalika, pasipo NEEMA huwezi kukubalika mbele za Mungu wala wanadamu, hata ungefanya jambo JEMA au ZURI kiasi gani.    • Ukiwa mahali ambapo umekwama kabisa NEEMA ndipo inapojitokeza na kukupa Msaada, NEEMA ndiyo inayoleta usaidizi, ili uweze kusaidiwa unahitaji NEEMA.     • Ukikosa NEEMA hata kama una sura nzuri haku...
Image
ZIARA YA KITUME NA KINABII MKOA WA KIGOMA. SOMO: NEEMA YA BWANA YESU. NEEMA ndiyo inayomfanya shetani apige KELELE, siyo Nguvu ya Mungu kwa sababu Nguvu ya Mungu anaijua, na ilikuwepo hata kabla ya kuasi kwake, lakini hakujua NEEMA. Siku alipokutana na NEEMA; na Akaijua ndipo alipopiga Kelele, (Neema ni Bwana YESU). Yohana akasema “katika Yeye huyo vitu vyote viliumbwa” Neema ndiyo chanzo cha Imani, ni NEEMA pekee ndiyo inayoweza kufanya Maajabu ndani ya mtu na katika Maisha yake. Huwezi kumshinda mtu mwenye NEEMA kwa sababu Bwana YESU alikufa kwa ajili yake na akampa hiyo NEEMA. NEEMA hufanya Kazi mahali pale ambapo ustahili haupo, hicho ndicho shetani Anakiogopa na Kulalamika, kwa sababu kabla ya NEEMA kuja sisi tulikuwa wenye dhambi, hivyo yeye alikuwa anafurahia kwani aliweza kufanya chochote anachojisikia katika Maisha yetu. Lakini baada ya Neema kutujia tukaokolewa na kufanyika kuwa wenye haki wa Mungu, yeye tena akawa hana nafasi katika Maisha yetu. Yeye alikuwa anatum...
Image
ZIARA YA KITUME NA KINABII MKOANI KIGOMA. PICHANI: Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira na Mama Eliakunda Mwingira walipokuwa wakiwasili Efatha Ministry KIGOMA. Katika kuwasili kwao kuliambatana na UFUNGUZI wa Kituo kikubwa (Kituo Mama) cha Mkoa wa Kigoma, kilichopo Kigoma mjini maeneo ya Ujenzi, kinachoongozwa na Mchungaji Kiongozi Benson Mpelle. Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira aliweka WAKFU JENGO hilo tayari kwa ajili ya matumizi ya IBADA.
Image
Naibariki Alhamisi yangu, Alhamisi yangu IMEBARIKIWA, Nami NIMEBARIKIWA, USHINDI wangu UMEBARIKIWA, Kazi zangu ZIMEBARIKIWA, Biashara zangu ZIMEBARIKIWA, Utumishi wangu UMEBARIKIWA, Masomo yangu YAMEBARIKIWA, Watoto wangu WAMEBARIKIWA, Mke wangu/ Mume Wangu AMEBARIKIWA, Wokovu wangu UMEBARIKIWA, Utulivu wa MOYO wangu UMEBARIKIWA, YESU Wewe ni MZURI BWANA, Nakupenda YESU, Haleluya.