SOMO: NEEMA YA BWANA YESU.

ZIARA YA KITUME NA KINABII MKOA WA KIGOMA.
SOMO: NEEMA YA BWANA YESU.
NEEMA ni ya Bwana YESU, UPENDO ni wa Mungu BABA na USHIRIKA ni wa ROHO MTAKATIFU.
NEEMA ni Nini? Neema ni kitu ambacho mtu Anaweza kukipata pasipo kustahili. Tumeokolewa kwa Neema, sisi tulikuwa ni wenye dhambi na wala hatukustahili kuokolewa, lakini kwa Neema ya Bwana YESU tumepata kuokolewa.
Kwa nini Neema? Neema ndiyo inayokufungulia ili uweze kufika mahali ambapo utakuwa na SHUKRANI kwa Mungu, bila Neema huwezi kuwa na SHUKRANI. Kwa nini mtu mwenye Neema anakuwa na Shukrani? Ni kwa sababu ametendewa kitu ambacho hakutarajia kukipata. Jambo lolote ambalo unalipata pasipo tarajio na likakupa wewe Ahueni, Nafuu au Faraja hiyo ndiyo inaitwa NEEMA.
Neema ni ya muhimu sana kwa mtu yeyote yule Anayetamani kwenda mbele, awe ameokoka au hajaokoka, mtu akishafikiwa na Neema anakuwa na Changamko katika Maisha yake na SHUKRANI kwa Mungu wake, bila NEEMA hakuna Changamko wala Shukrani.
ITAMANI NEEMA KATIKA MAISHA YAKO ILI UWEZE KUWA BORA.

:- MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA, EFATHA MINISTRY.

Comments