ZIARA YA KITUME NA KINABII MKOA WA KIGOMA.
SOMO: NEEMA YA BWANA YESU.
NEEMA ndiyo inayomfanya shetani apige KELELE, siyo Nguvu ya Mungu kwa sababu Nguvu ya Mungu anaijua, na ilikuwepo hata kabla ya kuasi kwake, lakini hakujua NEEMA. Siku alipokutana na NEEMA; na Akaijua ndipo alipopiga Kelele, (Neema ni Bwana YESU).
Yohana akasema “katika Yeye huyo vitu vyote viliumbwa” Neema ndiyo chanzo cha Imani, ni NEEMA pekee ndiyo inayoweza kufanya Maajabu ndani ya mtu na katika Maisha yake. Huwezi kumshinda mtu mwenye NEEMA kwa sababu Bwana YESU alikufa kwa ajili yake na akampa hiyo NEEMA.
NEEMA hufanya Kazi mahali pale ambapo ustahili haupo, hicho ndicho shetani Anakiogopa na Kulalamika, kwa sababu kabla ya NEEMA kuja sisi tulikuwa wenye dhambi, hivyo yeye alikuwa anafurahia kwani aliweza kufanya chochote anachojisikia katika Maisha yetu. Lakini baada ya Neema kutujia tukaokolewa na kufanyika kuwa wenye haki wa Mungu, yeye tena akawa hana nafasi katika Maisha yetu.
Yeye alikuwa anatumia uovu wetu kutushitaki kwa Mungu na kupata uhalali wa kututesa, lakini baada ya NEEMA kutujilia; akakuta tumeshasafishwa kwa Damu ya YESU KRISTO na tukawa wenye HAKI wa Mungu. Hiki ndicho kinacho mfanya ibilisi mpaka leo haelewi inakuwaje wenye dhambi wanakuwa wenye Haki kwa Mungu na ndiyo maana anapambana na hiyo NEEMA. Anabaki kupiga KELELE tu kwa sababu yeye hajapewa hiyo Neema na wala hatakaa aipate.
Neema ni nini? Neema maana yake ni mtu Aliyesamehewa na wala Hahesabiwi makosa.
Zaburi 32:1-2 “Heri aliyesamehewa dhambi, Na kusitiriwa makosa yake. Heri BWANA asiyemhesabia upotovu, Ambaye rohoni mwake hamna hila.” Mtu aliye na NEEMA hata akikosea inakuwa ni rahisi sana Kusamehewa.

:- MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA, EFATHA MINISTRY.

Comments