MCHUNGAJI DAVID MWAKISOLE 1korintho 12:1-3 “ Basi, ndugu zangu, kwa habari ya karama za roho, sitaki mkose kufahamu. Mwajua ya kuwa mlipokuwa watu wa Mataifa, mlichukuliwa kufuata sanamu zisizonena, kama mlivyoongozwa. Kwa hiyo nawaarifu, ya kwamba hakuna mtu anenaye katika Roho wa Mungu, kusema, Yesu amelaaniwa; wala hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu. ” Kunatofauti ya karama za rohoni, Kanisa la Mungu linapaswa kuishi kwa kuheshimiana, kwa mujibu wa Biblia inasema hakuna mtu kamili bali ni mimi na wewe tukigawiana karama na vipawa tulivyopewa na Mungu ndio tunakuwa kamili ndio maana tunafananishwa na mwili, mkono pekee hauwezi kuwa mwili mmoja bila mguu sikio kichwa na viungo vingine.
Posts
Showing posts from July, 2016
- Get link
- X
- Other Apps
USHUHUDA: Naitwa Godlynne William, napenda kumshukuru MUNGU kwa matendo yake makuu aliyonitendea katika elimu yangu. Nimemaliza kidato cha sita katika shule ya Canossa High School na nimepata Division 1.9 PCM. Nilikuwa natamani kusoma course ya petrochemical Engineering na MUNGU amenisaidia nimepata hiyo course na naenda chuo kikuu . Namshukuru sana MUNGU kwani ni kwa uweza na nguvu zake siyo kwa akili zangu.
- Get link
- X
- Other Apps
USHUHUDA Naitwa WillFred Kaaya, namshukuru Mungu kwa kuniponya kwani nilikuwa nasumbuliwa na Nimonia, ambayo ilinisumbua sana hata kufikia kutaka kukata tamaa, lakini Yesu alimtumia Mtumishi wake Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira alinitia moyo na kuniombea pamoja na watumishi wengine wa Efatha na sasa nimepona namtukuza Mungu, nilisimamia Neno kuwa sitakufa bali nitaishi, nawaomba watumishi wenzangu tusikate tamaa Yesu yupo pamoja nasi namtukuza MUNGU.
Haleluya wana wa MUNGU, Efatha Ministry Mwenge Dar es salaam Tanzania tunawakaribisha tena katika Ibada nzuri leo Jumapili tarehe 24/7/2017. Ibada ya kwanza inaendelea mahali hapa kwa wale mlioko mbali na Efatha Ministry mnaweza kufuatilia Ibada za siku ya leo kupitia www.mixlr.com/efatha-ministry .
- Get link
- X
- Other Apps