Praying always strengthen us.So keep praying do not get tired Pray always.

Sunday, March 30, 2014

IBADA KUU JUMAPILI 30/3/2014

Kipindi cha Shuhuda, Wana wa MUNGU walitoka mbele kushuhudia Matendo Makuu ya MUNGU Wetu MKUU Aliyowatendea katika Maisha yao...

 Wana kwaya "Mass Choir" wakiwa katika Uwepo wa ROHO MTAKATIFU MUNGU wakiimba na kuwasogeza Wana wa MUNGU mbele za BWANA

Kipindi cha Shukrani, Mwenyekiti wa Kamati wa za Kusanyiko Eng. Mwanukuzi alitoka mbele na Kamati yake ya Kusanyiko, kuja kutoa Shukrani kwa MUNGU BABA Yetu MKUU kwa yote Mema na Mambo Makuu Waliyotendewa toka walipoaminiwa na kukabidhiwa Jukumu hilo la kusimamia Kusanyiko, pia walikuja na Zawadi kwa Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira zawadi ya Kiti na Meza

Kamati ya Kusanyiko wakitoa Zawadi na kumkabidhi Mtumishi wa MUNGU Mama Eliakunda Josephat Elias Mwingira kwa niaba ya Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira.

 

Tuesday, March 25, 2014

ACHA NIKUIMBIE NA NIKUCHEZEE.

"WEWE ni MUNGU MTENDA MAMBO YOTE, Wewe ni MUNGU Mtenda mambo yote, Wewe ni MUNGU Ninakuinua hii leo, Wewe ni Mtenda mambo yote BABA, Tukikuita unaonekana BABA, Haleluya, Wewe ni MUNGU BABA, Acha nikuchezee BABA, WEWE Ndiwe MFALME, ndiwe MFALME Haleluya, Wewe JEMEDARI, JEMEDARI BWANA Haleluya."
Wednesday, March 12, 2014

SEHEMU YA MAHUBIRI YA IBADA YA JUMAPILI 9 March 2014

Mtumishi wa MUNGU Mkalimani wetu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.

"Katika Agano la MUNGU kwetu Mwaka huu amesema ni mwaka wa KIBALI, utaenda kuuona ukuu wa MUNGU, Mwanzo: 12:1-3 (BWANA Akamwambia Abramu …) MUNGU Anaongea na mtu wake “Toka”, na sio watu ila wewe. Ili uweze kuelewa ujumbe wa Kibali fanya KIBALI chako kiwe cha binafsi, Usifanye cha harambee, Kibali chako ni cha kipekee.

Kumbuka kuna mtu anashuhudia matendo makuu ya MUNGU aliyomtendea kila iitwapo leo maana yake amemfanya MUNGU kuwa ni wa kwake lakini wewe tangu ushuhudie mwaka juzi hujashuhudia tena, MFANYE MUNGU WA Kwako.

TOKA;
- Toka wewe katika Nchi yako - kuna tabia za kitaifa/ tabia za nchi zisizofaa, Toka katika hizo.
- Toka wewe katika jamaa zako - kuna tabia za jamii/ unawafahamu huko toka, TOKA katika tabia mbaya za jamaa zako unaowafahamu, wanaokuzunguka.
- Toka wewe katika nyumba ya baba yako – toka katika tabia za nyumba ya baba yako.

Kwa hiyo sisi hatuna haja ya kutoka nchini kwetu na kwenda ulaya kutumikishwa hiyo siyo akili nzuri. Walokole wengi wameokoka lakini “Kutoka” katika tabia za baba zao, nchi yako, jamaa yako bado hawajatoka, hilo ni tatizo, Bibilia inasema katika kitabu cha Amosi ‘Niondoleeni kelele zenu’ ni kweli unaweza kufunga kwalezima/ ramadhani, Bibilia inauliza ‘hiyo ndiyo saumu niliyokueleza’? Siku UTAKAPOTOKA katika TABIA za nchi yako, jamaa zako, Uzao wa baba yako nakuhakikishia MUNGU Atakuonyesha NJIA ya kwenda. Unapoamua KUACHANA na Tabia za nyumba ya baba yako, Jamaa zako, Nchi yako UTUKUFU WA MUNGU Utakuzunguka.

Mnasikia sana Mafundisho, Mahubiri lakini kuchukua hatua ya kutenda inakuwa kazi, nakumbuka mimi nilipoamua kutoka katika tabia za nchi yangu, jamaa zangu, na katika tabia za nyumba ya baba yangu, nilibaki peke yangu hata wale niliokuwa nasali nao walisema usifuatane na sisi wenye dhambi. Unapoamua kuachana na dhambi UTUKUFU WA MUNGU Unakufunika, hata nilipokuwa nasali KKKT nikisimama kuhubiri kweli ya MUNGU wazee wa kanisa wananitoa nje, maana walikuwa hawataki kunisikiliza niwaambie kile NINACHOELEKEZWA na MUNGU.

IBADA maana yake nini?, Ibada maana yake ni watu kupeleka MAHITAJI yao kwa MUNGU na MUNGU kuwajibu, Ibada sio Utakatifu, MUNGU hufanya mambo yake kwa sekunde chache inategemea ulivyojiandaa. Kutoka kuna gharama, MUNGU alimuambia “Toka” katika nyumba ya baba yako, Ibrahimu alipotoka akakosea akatoka na baba yake, lakini baba yake alifia njiani maana MUNGU haitaji mizigo!

TOKA; Ukishatoka ndio Anakuonyesha, ni kweli “Amekuokoa, Amekufungua, Amekuweka HURU”, lakini Anataka UTOKE."Monday, March 10, 2014

WHAT CAN CAUSE SUFFERING?

"What can cause suffering?
i. Personally.
ii. Your parents,
iii. GOD Himself.
iv. Satan

We read (Prov 16:4) “The LORD has prepared everything for His purpose; even the wicked for the day of disaster.” The wicked cannot be cured from his evil, no matter how much you pray for him. He remains evil to the day he dies, for it he is destined for evil. Some will come to church, and they will fast and pray with you, but their aim will be to deceive you.

GOD spoke to Jeremiah, “I knew you before you were conceived, and I chose and cleansed you. HE cleansed him for HE knew that there are problems that are inherited from the parents. You are born again, you became known to GOD before you were born again, and HE tagged you before you were born again. This is the reason you seek the LORD with tears.

JESUS asked, “Can a blind man lead other blind men”? Before you decide to follow a leader, first investigate his life; is it moving forward or is it moving backwards? Does he have the Knowledge of GOD or he doesn’t?

Every situation that we pass through has an origin; others you have caused on your own, in your own laziness, others by your parents and others GOD has allowed. It is good to understand where your problem arose from. The devil will only come when he sees that things are on his favor.

Example
The problems that GOD allows to happen are:-"...Teachings from Apostle & Prophet Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.

SAFARI KUTOKA NCHI TAKATATIFU ISRAEL

Pichani baadhi ya Ndugu, Jamaa na Marafiki pamoja na Watumishi wa MUNGU na Wana wa MUNGU wakiwa Uwanjani tayari kuwapokea Wenzetu toka Israel.

Pichani Mtangazaji wa Kituo cha Television cha EFATHA MINISTRY (TRENET Television) nao hawakuwa nyuma kurekodi na kurusha kilichokuwa kinaendelea Uwanjani hapo.

 Pichani Familia, Ndugu, Rafiki wakiwa na furaha kuwapokea Familia zao Wana wa MUNGU walipokuwa wakiwasili.

 Pichani Msafara ulianza kuelekea Kanisani EFATHA MINISTRY Mwenge.


 Pichani TRENET na EFATHA MINISTRY ICT hawakuwa nyuma nao katika kupata yote yaliyokuwa yakiendelea... wakiwa njiani wakielekea na Masafara Kanisani Efatha Mwenge.

 Pichani Watumishi wa MUNGU wakiwa wamejipanga kwa Furaha Kanisani EFATHA MINISTRY Mwenge (Sehemu ya Jengo la Ofisi Kuu) tayari kumpokea Mtumishi wa MUNGU Mkalimani wetu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira.

Haleluya... pichani Baba yetu wa Kiroho Mtumishi wa MUNGU Mbeba KUSUDI Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira akiwasili kanisani EFATHA MINISTRY Mwenge (Sehemu ya Kuingilia Ofisi Kuu Lounge) akipokelewa na Watumishi wa MUNGu Wachungaji na Wafanyakazi wa Ofisi Kuu.

 

 Pichani Mtumishi wa MUNGU Mama Eliakunda Josephat Elias Mwingira, akipokelewa kwa Furaha na Watumishi wa MUNGU Wachungaji na Wafanyakazi wa EFATHA MINISTRY Ofisi Kuu Mwenge, Haleluya...!

 Pichani Mtumishi wa MUNGU Mkalimani wetu Mbeba KUSUDI Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira akiwapungia Mkono na kuwasalimia Wana wa MUNGU kwa Furaha KUU wakati akiingia Ibadani.