NENO
Rumi 8:28 Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. Kusudi la Mungu kukuokoa ni ufanye KAZI pamoja naye ili akupe Mema ya Nchi, kwa muda mwingi sana umefanya kazi zako wewe mwenyewe, wakati mwingine umefanya kazi za shetani. Kwa ujumla Mungu amekusudia MEMA kwa kila ALIYEOKOKA na Mema haya yanapatika kwa KUFANYA KAZI. Bila kufanya kazi na Mungu huwezi kula Mema ya Nchi, yaani Utajiri aliouweka Mungu hapa duniani