SHUHUDA Jumapili tarehe 22/2/2015
Nilikuwa na Kibao cha Marufuku kwamba Siwezi kufaulu, lakini baada ya Kuomba na Kuvunja Kibao hicho, Nimefaulu na Nimepata DIVISION ONE. Ester David Msimbi: Napenda kumshukuru MUNGU, katika kusoma kwangu nimekuwa nikifanya vizuri lakini nilikuwa sishiki Nafasi ya Kwanza, nilikuwa namaliza Kisutu Sekondari, wakati huo nilikuwa na mambo yangu mengi ya uongozi, nilikuwa sifanyi vizuri, nilipokuwa nafanya Mitihani nilikuwa sipati zile Division zinazo takiwa. Lakini baada ya Mafundisho ya Mchungaji wangu Mama Mdadila aliposema kuna “KIBAO cha Marufuku” kimeandikwa mbele yangu kwamba Sitafaulu, akasema “TUKIVUNJE” kile kibao, na baada ya Kuomba na Kuvunja kile kibao MUNGU Aliniona na Kunisaidia, nimepata Division ONE. Na kuna maneno magumu kutoka kwa baba yangu mzazi alinitamkia, ya kwamba nitafeli nitapata ziro - ziro lakini MUNGU alijiinua kwangu na kunipa Kibali kwa Mwaka huu wa (Mtembeo Wa MUNGU Kwa Wale Alio Waridhia) nimepata Divison One. Lakini hii yote ni kwa sab...