Praying always strengthen us.So keep praying do not get tired Pray always.

Sunday, December 4, 2016

Naitwa Godluck Massawe: shuhuda1Namshukuru Mungu kwa kuniokoa katika ajali ya pikipili iliyotokea eneo la Ubungo, mimi nikiwa kwenye pikipiki mbele yangu kuna shimo kubwa lililochimbwa na watu wa Dawasco na upande mwingine kulikuwa na gari ambayo ilinifuata baada ya kuona lile shimo. Mwenzangu alinigonga nami niliumia mkono na vidole vitatu vilikuwa vimeumia na kimoja kikawa kinaninginia nilipelekwa Hospitali ya Mwananyamala walinipiga picha ya X-ray wakasema kidole kimevunjika, nikiwa hapo nikasikia sauti ikiniambia nenda kwa Mchungaji wako nilipofika kwa Mchungaji nikakuta kuna ibada ya Cell nami nikaungana nao na baadaye nikamweleza naye akaniambia neno moja unakubali kumtumikia Mungu nikajibu ndio, akaniombea na muda huo mkono ulikuwa umevimba lakini baada ya maombi nikaona maumivu yale makali yameondoka. Kesho yake nikarudi Hospitali na Daktari aliponiangalia mkono na ilepicha ya X- ray niliyopiga ile siku ya ajali ambayo ilikuwa inaonyesha nimevunjika cha kushangaza Daktari alisema sijavunjika wala sina kidonda, tayari YESU alikuwa ameniponya na sasa mkono ni mzima kabisa namtukuza Mungu kwa kuniponya. Siri moja inatupasa kufanya kazi ya Bwana kwa bidii nasi tutakuwa salama.

shuhuda1

Jina langu ni NEEMA KALUGULA naishi Holland nina kila sababu ya kumshukuru Mungu, mwaka 2005 nilimtolea Mungu kiwanja cha kujenga kanisa. Mume wangu akataka kuniacha kabisa. Mungu akaniambia usijali watoto wako watasoma Ulaya. Nikapata kazi mahakama ya kimataifa na watoto wangu wamesoma Ulaya na mmoja ameanza kazi. Namshukuru Mungu alichokisema kimetimia. Pia mwanangu alipata ugonjwa wa kuanguka na kuzimia nikatuma maombi PRAYER HOUSE, EFATHA MINISTRYMWENGE wakamuombea na sasa mtoto wangu ni mzima na anaendelea na kazi. Ni mengi amenitendea. NAMSHUKURU BABA MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA NA Wana maombi wa PRAYER HOUSE. MUNGU AWABARIKI SANA NI MIMI NEEMA KALUGULA. Kutoka HOLLAND.

dsc_7945

USHUHUDA Naitwa MACKDONALD MAANYA: Natoka eneo la Shalom zone ya Ebenezer, napenda kumshukuru MUNGU kwa yale aliyonitendea, ni mengi sana lakini kubwa kabisa napenda kumtukuza MUNGU kuhusu Ndoa yangu yametokea mambo Mengi na vikwazo vingi lakini nilisimama kwamba jambo hili lazima liwezekane na hatimaye tulifunga Ndoa Takatifu katika Madhabahu ya Efatha na pia Mungu ametujalia mapacha SHONE na SAMWEL. Namshukuru MUNGU kwani Mke wangu ananifanya Nang’ara, ukiona mimi Nang’ara basi ni Mke wangu. Wewe ambaye hujaoa ndoa sio yako ni ya MUNGU wala usione kuwa kufunga Ndoa ni ngumu.

MCHUNGAJI THADAYO MBAZI MSUYA. a10Uzima ni roho wa Mungu kupitia Yesu kristo yohana 1;3-5 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. Nayo nuru yang’aa gizani, wala giza halikuiweza. “ – Ndani ya neno ndimo ulipo uzima – Neno ni pumzi na neno ni roho, – Utajuaje huyu mtu anauzima 1. UPENDO ; kuna NENO ndani yake ili Mungu ajitwalie UTUKUFU na huo uzima uwe ni NURU ambao hawajaokoka lazima uwalete kwa Yesu, hata ukisema kwa lugha ya manabii kama huna upendo ni kazi bure. Kama ukiwa na chuki huwezi kusoma biblia na wala kitabu chochote cha Efatha . Yesu alijitoa ili mimi na wewe tuwe na upendo wa kweli. Mlete mtu kwa Yesu ili upendo wake ukamilike. 2. Unaposikia Neno la Mungu unapaswa kumsoma kwani yeye anapatikana kwenye Neno usiwe mvivu wa kusoma biblia huwezi kuwa na upendo lakini, ukiwa msomaji wa biblia utakuwa na sifa ya kuitwa mfalme na utakua na neema ya kumpenda mwenzako. Tunaye baba anayefichua ya sirini upendo wa Bwana lazima ujue Neno kwanza. 3. Kama huna upendo ndani ya Efatha wewe ni maiti. Unaheri wewe uliye okoka ili uende ukawapatie wengine Neema hiyo ifanyie kazi mtumishi wa Mungu. 4. Ili uweze kumpenda Yesu lazima usome neno asubuhi mchana na jioni, 5. kaa karibu na mtu anaye mpenda Mungu kaa vizuri kwa sababu upo sehemu salama. Mimi ni nani embu kubali kukaa ndani ya Efatha Tulia mbele za Bwana upate upendo wa kweli. Amina

a10

EFATHA MINISTRY MASS CHOIR, wakimtumikia MUNGU katika Ibada ya pili hapa Efatha Ministry Mwenge Dar es salaam Tanzania

Sunday, November 27, 2016

Mchungaji David Mwakisole: SOMO: ASILI YA BARAKA ZETU NI KATIKA KRISTO YESU: BWANA YESU ni RAFIKI yetu. Mfano:- Ukiwa na rafiki yako unakuwa unampenda na unatamani kumfurahisha mara zote, hivyo kama unatambua kuwa BWANA YESU ni RAFIKI yako unatakiwa UMFURAHISHE, Je utamfurahishaje? • Kwa kutenda sawasawa na maagizo yake kutoka kwa Watumishi wa Mungu, ukiwa unatamani kufanya mambo mazuri kwa ajili yake ndipo anafurahi na kama kunakitu kinakuzuilia ili usifanye vizuri anakiondoa na kukuacha ukiwa huru. • Tamani kufanya mambo mazuri kwa ajili YAKE ili YEYE akufurahie na kufungua yale yaliyofungwa katika maisha yako. Ukikosa kuzingatia kinachotoka katika MADHABAHU ya Mungu dunia itakupelekesha, unapofika hemani mwa BWANA (Kanisani) unatakiwa kutafakari yanayotoka katika MADHABAHU, usiwaze tofauti na NENO linalotoka katika MADHABAHU ya BWANA maana hautapokea chochote na mwisho wa siku utatoka kama ulivyoingia.

Mchungaji David Mwakisole: SOMO: ASILI YA BARAKA ZETU NI KATIKA KRISTO YESU: Ili tuweze kuvuta BARAKA za MUNGU kwetu ni lazima tuwe na kitu cha kumpa MUNGU, tusiende mbele zake mikono mitupu, toa nguvu zako na mali zako, baraka haziji mpaka UMEFANYA KWA BIDII ndipo wale malaika waliotumwa kwako wanapopata nguvu ya kuvuka vizuizi na kukuletea BARAKA zako. Unapokuwa na AMANI ya YESU ndipo unaweza kuzalisha vitu vingi katika maisha yako. Ili shetani akuweze kitu cha kwanza anakuondolea AMANI kwa kukukumbusha yaliyopita. Ni kweli ulikuwa mwizi, mzinzi, mlevi lakini mara baada ya kuokoka YESU alisamehe yote sasa shetani asikukumbushe ya nyuma.