Posts

Showing posts from July, 2013

JUMAPILI YA UIMBAJI NA KUCHEZA MBELE ZA BWANA

Image
   Kabila la wapogoro wakiimba na kucheza ngoma ya asili yao wakimtukuza MUNGU. Kabila la Wachaga wakimtukuza MUNGU kwa kuimba na kucheza kwa ngoma ya asili yao ya kichaga,Duhhh kwa YESU raha sanaaa vya mwilini tukivirudisha rohoni mambo yanapendeza kabisaa,na Bwana Mungu anatufurahia.  Kabila la wahaya nao wakasema hapana na sisi tutamtukuza Bwana MUNGU wa majeshi aliyetuokoa na kutupigania bila ushuru wowote,wakicheza ngoma ya asili ya kihaya. Mama nae hakuwa nyuma kuwakilisha kabila lake,Wameru hao wakiwakilisha. Kabila la wagogo nao wakicheza ngoma ya kigogo huku wakimsifu bwana  MUNGU.Mama huyu alijituma sana kuonyesha ile asili ya ndani kabisa ya wagogo,safi sana. Wenye mji wao hao wakiwakilisha kumtukuza Bwana wetu YESU,Wazaramo hao.