Tuliotendewa na Yesu wetu huyu wa Efatha ni makuu jamani,ni makuu ziwezi kueleza.Tukibubujika ni haki yetu maana mioyo yetu ikiwa cha kulipa kwa aliyetundea inaona hamna,tunabaki tukibubujika.
Wana wa Efatha wakijipatia uji safiii,zawadi toka kwa baba jioni baada ya mfungo wa siku nzima. Na maandazi kwa wingiii.Ni furaha kukutanika pamoja wana wa BABA aliye juu na kupata mlo pamoja.Wadau niwaulize hivi na mbinguni si itakuwa ni hivihivi aaaaaa No ni zaidi ya hivi wapenzi.Wote mlio nje ya YESU karibuniiii maana hiii ni zaidi ya ubwete ubwete kama Baba yetu Elias Mwingira asemavyo kuwa tutakula kwa ubwete ubwete.
Kwa yesu rahaa,hakuna magonjwa,hakuna vilio hakuna masumbuko.Mwana wa MUNGU akishuhudia jinsi Mungu alivyomtendea maajabu.Kwa wale wenye imani haba amewaletea utrasound kwa uhakikisho.Halafu nitoke kwa YESU,mwanaume wa wanaume niende kwa nani mimi????