A LIFE OF SALVATION

 


The Life of Salvation is not the same, everyone acts differently from the other and has his own mountain to climb. The Life of Salvation is like a body with many organs and does not perform one function (Romans 12: 4). Everyone does different things, each has his own mountain to climb.

Jesus has saved us and given us to serve in various positions within the Kingdom of God. You should not complain about the difficulty of your journey in your ministry because that is your responsibility. If you encounter challenges in your ministry do not give up it is good to fight to the end. Do not give up because the devil has attacked you and thrown you out. The defeated will not enter heaven but the victors. Those who fail even if they speak in tongues will not enter Heaven.

Sometimes the devil may tempt you to choose a job which do not have many challenges with people and give up what you are supposed to do, do not agree with him but do the work you were meant to do even if it has many challenges because when you win, you win with Christ. Do not allow the devil to take you out of your God-given position for any reason, for a work without challenges is not victorious.

We are called in the midst of the enemy so wanting an easy job is not God's call. God's call to us is in the midst of wolves and you are a sheep who is their food. That's where our cup overflows so agree to die there. Do not desire to do God's work in an easy place. If God gives you the desire to support His work with your money and possessions, do so without being pushed.

Prayers:

·         Heavenly Father, guide my heart.

Swahili Translation:

SOMO: MAISHA YA WOKOVU.

Maisha ya Wokovu hayafanani, kila mtu anatenda tofauti na mwingine na ana mlima wake wakupanda. Maisha ya Wokovu ni sawa na mwili ulivyo na viungo vingi wala havitendi kazi moja (Warumi 12:4). Kila mtu anatenda mambo tofauti kila mmoja ana mlima wake anaopaswa kupanda.

Yesu ametuokoa na kutupa kutumika katika nafasi mbalimbali ndani ya Ufalme wa Mungu. Hupaswi kulalamikia ugumu wa mapito yako katika Utumishi wako maana hilo ndilo fungu lako. Ukikutana na changamoto katika Utumishi wako usiache ni vizuri ukapambana hadi mwisho. Usishindwe kwa sababu shetani amekushambulia na kukurusha nje. Mbinguni hawataingia walioshindwa bali wataingia walioshinda. Walioshindwa hata kama wananena kwa lugha mpya hawataingia Mbinguni.

Wakati mwingine shetani anaweza kukushawishi uchague kazi ambayo haina misuguano mingi na watu na uache uliyopaswa kufanya, Usikubaliane naye bali fanya kazi ile uliyokusudiwa hata kama ina changamoto nyingi kwa sababu utakaposhinda, utakuwa umeshinda pamoja na Kristo. Usimruhusu shetani akuondoe kwenye nafasi uliyopewa na Mungu kwa sababu yoyote, maana kazi isiyo na changamoto haina ushindi.

Tumeitwa katikati ya adui kwa hiyo kutaka kazi nyepesi, huo siyo wito wa Mungu. wito wa Mungu kwetu uko katikati ya mbwa mwitu na Wewe ni kondoo ambaye ni chakula chao. Hapo ndipo kikombe chetu kinafurika kwa hiyo kubali kufia hapo. Usitamani kufanya kazi ya Mungu katika nafasi nyepesi. Mungu akikupa msukumo wa kusaidia kazi yake kwa mali na fedha zako, fanya hivyo pasipo kusukumwa.

Maombi:

• Baba wa Mbinguni naomba uongoze Moyo wangu.

By Servant of God Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira, Efatha Church.  

Comments