THE WORD OF GOD WILL TAKE AWAY YOUR SORROW

 


Sorrow overwhelms many people and makes them feel inferior and poor than others.

1 chronicles 4: 9- 10 “Now Jabez was more honorable than his brothers, and his mother called his name [a]Jabez, saying, “Because I bore him in pain.”…”

People who are in sorrow are many. One will know that he is under the spirit of sorrow by seeing that he is neither happy nor excited and all his things have no glory or strength, his activities are unprofitable.
While some enjoy life and afford many things; he cries and can do nothing. Sorrow always brings a lot of pain and crying because there is no guarantee of one's future. It makes him feel inferior and poor before others. The hope of getting out of this situation is for the person to ask himself if he is keeping the Word of God in his heart.

Psalm 119: 11 “Your word I have hidden in my heart, That I might not sin against You.”

A person who is in sorrow should turn his heart to the Word of God to get understanding. When a person finds out the cause of his or her grief, he or she should look for a Word in the Bible that gives him or her permission to pray, depending on the circumstances. In each case there is a special Word for it.

Psalm 119: 133 “Direct my steps by Your word, And let no iniquity have dominion over me.”

Let him take the Word that speaks of his condition as his place of authority. Let him go to the Word and not follow his own thoughts. The person should also consider his ways and circumstances and then make a decision to follow God and God will do something to that person

Swahili Translation:

Hali ya huzuni huwakandamiza watu wengi na kuwafanya wajione wanyonge na duni kuliko wengine.

1 Nyakati 4: 9- 10 "Naye Yabesi alikuwa mwenye heshima kuliko nduguze; na mamaye akamwita jina lake Yebesi, akisema ni kwa sababu nalimzaa kwa huzuni......."

Watu walio katika hali ya huzuni ni wengi. Mtu atajua yuko chini ya roho ya huzuni kwa kuona hana furaha wala changamko na mambo yake yote hayana utukufu wala uimara. Shughuli zake hazina faida. Wakati wengine wanafurahia maisha na kumudu mambo mengi; yeye hulia na hawezi. Mara zote huzuni huleta maumivu na kilio kingi maana hakuna uhakika wa ubaadaye wa mtu. Humfanya kujiona mnyonge na duni kuliko wengine. Tumaini la kutoka katika hali hii ni muhusika ajiulize kama anatunza Neno la Mungu moyoni mwake.

Zaburi 119: 11 " Moyoni mwangu nimeliweka Neno lako, Nisije nikakutenda dhambi",

Mtu mwenye huzuni anatakiwa aelekeze moyo wake kwenye Neno la Mungu ili apate ufahamu, muhusika anapobaini sababu ya huzuni yake, atafute Neno katika Biblia linalompa kibali cha kuomba, kulingana na hali anayopitia. Katika kila hali kuna Neno maalum kwa ajili yake.

Zaburi 119: 133 "Uzielekeze hatua zangu kwa Neno lako, Uovu usije ukanimili." 

Achukue hilo Neno linalozungumzia hali yake liwe mahali pake pa kusimamia. Aende kwa Neno wala asifuate mawazo yake mwenyewe.Pia mtu huyo hupaswa kutafakari njia zake na hali yake alafu afanye maamuzi ya kumfuata Mungu naye atafanya jambo kwake.

 By Servant of God Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira, Efatha Church.  

Comments