LOVE ALLOWS RELATIONSHIP TO BE KEPT.

 


When you are in love with someone there is a way to keep the relationship between you so that your friendship will last. You do this by being careful not to offend the one you love. If you love God you will serve Him happily even though the relationship must bring you pain first and that is the measure of your love for Him.

If you serve God easily, understand that you do not yet love Him. For example; the life of the Lord Jesus was not smooth from his birth to his death. Each step was like climbing a steep mountain. Herod wanted to kill Him, so He escaped to Egypt. When He wanted to start His work He was taken to the mountain and fast for forty days and there He was tempted by devil but He won. His ministry was difficult and extremely challenging. He often went to the mountain to pray. The glorious revelation of His image took place on a mountain. When He was arrested and tortured, even death on a cross took place on a mountain.

The comfort in pleasing God is that when you finish His work He will wipe away your tears. It is because the work of salvation is a battle of faith to get people out of Satan's dominion and take them into God's kingdom.

Swahili Translation:

UPENDO HUWEZESHA KUTUNZA MAHUSIANO.

Unapopendana na mtu kuna hali ya kutunza mahusiano kati yenu ili urafiki wenu udumu. Unafanya hivyo kwa kuwa mwangalifu ili usimkosee yule unayempenda. Ukimpenda Mungu utamtumikia kwa furaha ingawa nilazima uhusiano wako ukuvute kwenye maumivu kwanza na ndicho kipimo cha upendo wako kwake.

Ukimtumikia Mungu kwa urahisi elewa kuwa bado hujampenda. Kwa mfano; Maisha ya Bwana Yesu hayakuwa laini kuanzia kuzaliwa kwake mpaka kufa kwake. Kila hatua ilikuwa ni kama kupanda mlima mkali. Herode alitaka kumuua akatoroshwa kwenda Misri. Alipotaka kuanza kazi yake alipandishwa mlimani na kufunga siku arobaini na huko alijaribiwa na shetani lakini akashinda. Utumishi wake ulikuwa mgumu na wenye upinzani mwingi. Mara nyingi alikwenda mlimani kuomba. Kufunuliwa kwa utukufu wa sura yake kulifanyika mlimani. Alipokamatwa na kuteswa hata kufa msalabani kulifanyika mlimani.

Faraja iliyopo katika kumpendeza Mungu ni kuwa ukimaliza kazi yake atakufuta machozi. Ni kwa sababu kazi ya wokovu ni vita vya imani ili kuwatoa watu kwenye milki ya shetani na kuwapeleka kwenye milki ya Mungu.

 By Servant of God Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira, Efatha Church.  

Comments