JESUS CHRIST IS A GIFT


Jesus Christ is a gift because He came to earth for you. When you receive a gift you must open it and look at it to see what kind it is. Therefore, if you have accepted Jesus as Lord and Savior of your life you have received a gift from God. Inside the gift there is everything you need. You have to open it to receive what you want. When you open your gift and recognize it you find peace and victory in your life.

Question: Have you opened your gift and seen what it contains?

Inside that gift is the Mighty God. From the moment you received Jesus Christ as a gift you gained power to be victorious. By using that power you can do whatever you want and win. You can own your spirit world and the devil will not overpower you.

If you receive Jesus as a gift, you will receive an eternal Father, for God cares for His people forever; so everything you do will last forever. When you do things and they fail don't give up because it is those things which have failed and not you. If you know that, you will do it again and again until you succeed. The Bible says try everything and choose the right one.

Swahili Translation:

YESU KRISTO NI ZAWADI

Yesu Kristo ni zawadi kwa sababu alikuja duniani kwa ajili yako. Unapopokea zawadi ni lazima uifungue na kuiangalia ili ujue ni ya aina gani. Hivyo basi, kama umempokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako umepokea zawadi kutoka kwa Mungu. Ndani ya hiyo zawadi kuna kila kitu unachohitaji. Unapaswa kuifungua ili upokee unachotaka. Unapoifungua hiyo zawadi yako na kuitambua unapata amani na kuwa mshindi katika maisha yako.

Swali: Je, umeifungua hiyo zawadi yako na kuangalia ina nini?

Ndani ya hiyo zawadi kuna Mungu mwenye Nguvu.Kuanzia ulipompokea Yesu Kristo kama zawadi ulipata nguvu ya kuwa mshindi. Kwa kutumia nguvu hiyo unaweza kufanya jambo lolote unalotaka na kushinda. Unaweza kumiliki ulimwengu wako wa roho na shetani hatakuweza.

Ukimpokea Yesu kama zawadi, unampata Baba wa milele, kwa kuwa Mungu hujali watu wake milele; hivyo basi kila utakachofanya kitadumu milele. Unapofanya mambo yakakwama usikate tamaa kwani mambo hayo ndiyo yameshindikana na siyo wewe. Ukifahamu hivyo, utafanya tena na tena mpaka ufanikiwe. Biblia inasema jaribuni mambo yote na chagua lililo jema.

 By Servant of God Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira, Efatha Church.  

Comments