JESUS ​​CHRIST CAME TO MAKE YOU HAPPY.

 


He is a gift from God (Romans 5:15). When someone gives you a gift, his goal is to make you happy. The Lord Jesus removes everything that gives you pain and suffering so that you can be happy. He takes away your griefs and carry your sorrows so that evil may not overtake you.

He was wounded for your transgressions, he was bruised for your iniquities, the chastisement of your peace was upon him and with his stripes you were healed. You need healing of everything such as health, income, marriage, offspring, work, behavior and relationships.

Do you know that Jesus Christ is your happiness?

Success and wealth are not money but what you know. For example; couple's first gift in their lives is themselves. If each one makes the other live in peace God will teach him/her how to open other gifts. Moreover, if they don’t go along, God will not give them gifts because they will not be able to keep them. If one spouse is abusive, the abused spouse should go before the cross and make a statement and the abuser will be caught on the cross.

Swahili Translation:

YESU KRISTO ALIKUJA KUKUFURAHISHA.

Yeye ni zawadi na kipawa toka kwa Mungu (Warumi 5:15) Mtu anapokupa zawadi lengo lake ni ili wewe ufurahi. Bwana Yesu huondoa kila kitu kinachokupa maumivu na machungu ili uwe na furaha. Huyachukua masikitiko yako na kujitwika huzuni zako ili mabaya yasikupate.

Alijeruhiwa kwa makosa yako na kuchubuliwa kwa maovu yako alipata adhabu ya amani yako na kwa kupigwa kwake umepona.Unahitaji uponyaji wa kila kitu kama vile afya, kipato, ndoa, uzao, kazi, tabia na mahusiano.

Je, unajua kuwa Yesu Kristo ni furaha yako?

Mafanikio na utajiri sio fedha bali ni kile unachofahamu. Kwa mfano; zawadi ya kwanza ya wanandoa katika maisha yao ni wao wenyewe. Kila mmoja akimfanya mwenzake aishi kwa amani Mungu atamfundisha namna ya kufungua zawadi zingine. Aidha, kama hawapatani Mungu hatawapa zawadi kwa sababu watashindwa kuzitunza. Mwanandoa mmoja akiwa mkorofi anayeonewa apeleke hoja msalabani na huyo mkorofi atanaswa na huo msalaba.

 By Servant of God Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira, Efatha Church.  

Comments