THINGS TO CONSIDER IN ORDER TO ACHIEVE YOUR GREATNESS


People who have money get tired in their bodies but their minds get stronger. A poor person gets tired in the body and his mind becomes weak which is why he becomes very talkative. The Lord Jesus gave a parable about the rich man who gave his three slaves talents. The one who was given one talent did a great job and caused his body to be tired by burying that talent and as a result it produced nothing.

That is how sinners are, they always seek to blame others first instead of fulfilling their duty because they have a spirit of jealousy and selfishness. Man of God, use your mind and stop complaining.

Ask yourself, what did you do with what God has done for you, because whatever God has done for you, you can also help another. Some people have been healed of diseases, but they have not prayed for someone else to be healed. How will God provide for you physically when spiritually you do not want to share, or keep His purpose? That is why the Lord Jesus says "Hold fast what you have." he also said, "You have been given free, give free."

With the mind of Christ, we will be very rich as for God gives to the one who pleases Him, wisdom and knowledge, that he may work according to the desire of his heart and that it may fill his treasure. We have to teach people what we are commanded so that they too can teach others.

Swahili Translation:

Watu wenye fedha, huchoka akili lakini mwili unakuwa na nguvu. Mtu maskini, huchoka mwili na akili inakuwa dhaifu, ndio maana anakuwa muongeaji sana. Bwana Yesu alitoa mfano wa tajiri, aliyetoa talanta kwa watu wake wa tatu. Yule aliyepewa talanta moja, alifanya kazi kubwa na kuuchosha mwili wake; kwa kuizika hiyo talanta na matokeo yake hakuzalisha kitu.

Ndivyo walivyo wenye dhambi, siku zote wakosaji wanatafuta kulaumu wengine kwanza, badala ya kutimiza wajibu wao maana wana roho ya wivu na ubinafsi. Mtu wa Mungu tumia akili yako na acha kulalamika.

Je! yale uliyotendewa na Mungu umeweza kumsaidia na mwingine? Watu wengine wameponywa magonjwa, lakini hawajamwombea mtu mwingine ili naye apone. Mungu atakupaje vya mwilini wakati vya rohoni hutaki kugawa, wala kutunza kusudi lake? Ndio maana Bwana Yesu anasema "Shika sana ulicho nacho." pia akasema "Mmepewa bure toeni bure."

Tukiwa na ile nia ya Kristo, tutakuwa matajiri wakubwa, maana Mungu humpa yeye aliyemridhia, hekima na maarifa, ili afanye kazi apate haja ya moyo wake na ndiko kujaza hazina yake. Tunatakiwa kuwafundisha watu yale ambayo tumeamriwa ili na wao wawafundishe wengine.

By Servant of God Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira, Efatha Church.  

Comments